Serikali ya Ivory Coast imetangaza siku tatu za maombolezo ya
kitaifa baada ya zaidi ya watu sitini kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kwa
kukanyagwa wakati wa onyesho la fataki kuukaribisha mwaka mpya katika mji mkuu
wa Abidjan.
Kuna ripoti za kutatanisha kuhusu kilichosababisha maafa hayo karibu na uwanja wa michezo uliopo mjini Abidjan.
Baadhi ya wale walioshuhudia kisa hicho wanasema watu waliingiwa na wasiwasi baada ya vijana waliokuwa wamejihami kwa visu kuanza kuiba simu za mkononi huku wengine wakisema ni utepetevu wa maafisa wa usalama katika kuthibiti umati.
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouatarra, amewatembelea hosipitalini baadhi ya wale waliojeruhiwa na kusema kuwa kutakuwa na uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ambacho alikitaja kuwa mkasa wa kitaifa.
No comments:
Post a Comment