
David Cecil akiwa korokoroni
Mahakama moja nchini Uganda, imefutilia mbali kesi dhidi ya
mwandishi mmoja wa michezo ya tamthilia, David Cecil, ambaye alikuwa akikabiliwa
na shtaka la kuonyesha mchezo kuhusu hali ya wapenzi wa jinsia moja, katika mji
mkuu wa nchi hiyo Kampala.
Bwana Cecil, alikabiliwa na tuhuma za kukiuka sheria kwa makusudi.
Bwana Cecil ameiambia BBC, kuwa kesi hiyo ilifutiliwa mbali kutokana na kile
alichokitaja kama ukosefu wa ushahidi wa kutosha dhidi yake.
Mapenzi ya jinsia moja imeharamishwa nchini Uganda.
Bunge la nchi hiyo linajadili uwezekano kwa kuimarisha adhabu ya wale watakaopatikana wakijihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Rais wa Uganda akikagua gwaride la kijeshi
Alipigwa faini ya laki tano pesa za Uganda, sawa na dola mia mbili za Marekani.
Akiongea muda mfupi baada ya kesi dhidi yake kufutiliwa mbali Bwana Cecil alisema kuwa amefurahishwa na uamuzi huo, licha ya hofu kuwa huenda akafunguliwa mashtaka mengine.
Wakati huo huo, Wabunge wa Uganda, wanajaribu kuitisha Bunge likatishe kipindi cha mapumziko ili lijadili kukamatwa kwa baadhi ya wabunge kuhusiana na kifo cha mbunge mwanamke wa wilaya ya Butaleja, mashariki mwa Uganda, wiki mbili zilizopita.
Kifo hicho kimezusha hofu na mabishano ya kikatiba baina ya Rais Yoweri Museveni na wabunge.
Ili kufanikisha ombi hilo, inapasa kwa uchache wabunge 125 walitie sahihi na kisha kulifikisha kwa Spika, mwenye uwezo wa kulirudisha Bunge
No comments:
Post a Comment