Meneja wa Idara ya Biashara ya Barua, Fadya Zam (wa tatu kushoto), akiwaelezea wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, kazi zinazofanywa na idara hiyo, wakati wajumbe hao, walipokuwa wakitembelea mtandao wa Shirika la Posta Tanzania ili kujionea utendaji wa idara na vitengo mbalimbali, jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Meneja Mifumo ya Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania, David Mtake (kulia), akiwapatia maelezo Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo, kuhusu mfumo wa huo, unavyofanyakazi, wakati wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, walipokuwa wakitembelea mtandao wa Shirika la Posta Tanzania ili kujionea utendaji wa idara na vitengo mbalimbali, jijini Dar es Salaam jana.
Mmoja wa Wajumbe wa Bodi hiyo, Profesa Nicholas Bangu, akitaka ufafanuzi kuhusu ufanisi na utendaji wa kitengo cha Mauzo ya Stempu, wakati wajumbe hao, walipotembelea kitengo hicho, katika ziara hiyo jana.
Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme, akiwafafanua Wajumbe wa Bodi ya shirika hilo, masuala mbalimbali kuhusu mambo ya stempu, wakati wajumbe hao, wakiwa katika kitengo hicho kwenye ziara hiyo.
Kaimu Meneja Msaidizi wa Kitengo cha EMS, Conrada Makumbi, akitoa maelezo kwenye kikao na Wajumbe wa bodi hiyo, katika ziara hiyo.
Meneja wa Posta wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lawrance Mwasikili, akiwapatia maelezo wajumbe wa bodi katika kikao hicho cha pamoja.
Postamasta Mkuu, Deos Mndeme, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Yamungu Kayandabila (katikati), akizungumza katika kikao hicho cha pamoja na wakuu wa vitengo wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa bodi, Khadija Said Omar na kulia ni Postamasta Mkuu, Deos Mndeme.
Makamu Mwenyekiti wa bodi, Khadija Said Omar, akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Meneja wa Posta wa Mkoa wa Dar es Salaam, Lawrance Mwasikili, akiwaelezea Wajumbe wa bodi hiyo, jinsi uchambuzi wa barua za kwenda nchi mbalimbali unavyofanyika mkoani Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi wa Kaunta, mkoani Dar es Salaam, Hudson Mwakitalu, akiwapatia maelezo wajumbe hao wa Bodi ya Shirika, walipofika kitengo hicho.
Wajumbe wa bodi ya Shirika wakijadili jambo wakati walipokuwa kwenye ketengo cha Kaunta, Posta Kuu ya Dar es Salaam jana.
Meneja Mkoa wa Dar es Salaam, Lawrance Mwasikili, akifafanua jambo kwa wajumbe hao, walipokuwa kwenye kitengo hicho cha Kaunta.
Meneja Mkoa wa Dar es Salaam, Lawrance Mwasikili, akiwaelezea wajumbe hao, ratiba za usafirishaji barua za kwenda nchi mbalimbali duniani, wakati wakiwa Posta Kuu, Dar es Salaam jana.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika, wakiangalia kumbukumbu ya majina ya Askari wa Kijerumani, waliopigana Vita ya Kwanza ya Dunia yaliyoko kwenye jengo la Posta ya Zamani. Jengo hilo ndilo lililokuwa Makao Makuu ya Posta kwa nchi za Tanganyika, Rwanda na Burundi, wakati wa Utawala wa Kikoloni wa Kijerumani.
Viongozi wa Shirika la Posta wakipata viburudisho, baada ya ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment