TANGAZO


Wednesday, January 30, 2013

Tunisia yabunduliwa nje ya AFCON


Wachezaji wa Tunisia
MECHI ya mwisho ya makundi kati ya Togo na Tunisia, moja ya mechi ngumu zaidi katika fainali za mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu imekamilika.
Timu hizo mbili zimetoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja na hivyo Togo imefuzu kutokana na idadi ndogo ya magoli waliyofungwa katika raundi hiyo ya kwanza, licha kuzoa alama nne sawa na Tunisia.
Tunisia ilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili ifuzu kwa raundi ijayo huku togo nikihitaji sare ya aina yoyote ili kufuzu kwa raundi ijayo.
Togo ilianza mechi hiyo kwa vishindo huku ikipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 12 kupitia kwa mchezaji Serge Gakpe ambaye alipokea pasi nzuri kutoka kwa nahodha wa timu hiyo Emmanuel Adebayor.
Kunako dakika ya 30 Tunisia ilizawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya mshambuliaji wake Walid Hichri kuangusha kwenye eneo la hatari na Dare Nibombe.
Emmanuel Adebayor alipoteza nafasi nzuri sana dakika za mwanzo mwanzo za mechi hiyo na kadri mechi inavyoendelea, ndivyo wachezaji wa Tunisia wanvyoendelea kuimarika.
Khaled Mouelhi, ndiye aliye tunukiwa jukumu hilo la kuupiga mkwaju huo na bila ya kusita akaupachika wavuni, na kwa mara nyingine kufufua matumaini ya Tunisia ya kufuzu kwa robo fainali.
Baada ya dakika za kwanza 45, timu hizo mbili zilitoshana nguvu.
Tunisia ilianza kipindi cha pili huku ikiwa na nguvu zaidi na nusura ifunge bao la pili lakini mshambuliaji wake Oussama Darragi aliangushwa na Vincent Bossou.
Wachezaji wa Tunisia walimtaka refa wa mechi hiyo kuwapa penalti lakini ombo lao lilikataliwa baada ya muamuzi huyo kuamua hawakustahili.
Kocha wa Tunisia Sabi Trabelsi alifanya mabadiliko kadhaa ili kuongeza nguvu kikosi chake.
Kocha huyo alimuondoa mshambuliaji wake mmoja Wahbi Khazri na mahala pake kuchukuliwa na Zouheir Dhaouadi ambaye anaweza kuchezakucheza safu ya kati na ushambuliaji.
Dakika ya sabini na nane, Tunisia ilipoteza nafasi nzuri ya kufunga bao la pili, pale mchezaji wake alipopoteza kwaju wa penalti.
Wachezaji kadhaa wa Togo walipinga uamuzi huo wa refa hatua iliyopelea watatu kupewa kadi ya njano, Jonathan Ayite, nahodha Emmanuel Adebayor na kipa Kossi Agassa.
Tunisia, iliendeleza mashambulio yao dhidi ya Togo lakini juhudi zao ziligongwa mwamba na hivyo Togo kuandikisha historia ya kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment