TANGAZO


Wednesday, January 30, 2013

Shell haina hatia ya mafuta kuvuja Nigeria



Wakulima walioshtaki kampuni ya Shell
Mahakama nchini Uhlaonzi imetupilia mbali madai 4 kati 5 yaliyokuwa yamewasilishwa dhidi ya kampuni ya mafuta ya Shell, kuhusiana na kuchafua mazingira katika eneo lenye mafuta la Niger Delta.
Lakini iliipata tawi la kampuni hiyo nchini Nigeria kuwa na hatia ya uchafuzi wa mazingira na kuitaka kumlipa fidia mkulima mmoja wa Nigeria.
Kiwango cha athari za uchafuzi wa mazingira kiitaweza kutolewa baadaye.
Kesi hiyo ni ya kwanza kuwahi kuwasilishwa dhidi ya kampuni kubwa ya mafuta na wakulima wanne pamoja na shirika moja la kutetea mazingira la(Friends of the Earth.)
Kesi hiyo imehusishwa na uvujaji wa mafuta uliotokea katika maeneo ya Goi, Ogoniland; Oruma in Bayelsa State na katika jimbo lengine la tatu la Akwa

Wakulima walidai kuwa mafuta hayo yaliathiri mashamba yao na vidimbwi vya samakii

Hatma ya kesi hiyo inatazamiwa kutoa mwelekeo katika kesi zingine nyingi kama hiyo. Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni kubwa ya kimataifa ya mafuta kushitakiwa kwa uharibifu wa mazingira hasa katika nchi za nje ya Uholanzi.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na wanaharakati wa kutetea mazingira (Friends of the Earth,) pamoja na raia wanne wa Nigeria waliotaka kulipwa fidia kwa hasara waliyopata.
Wanne hao ambao ni mkulima na mvuvi, wanasema kuwa mafuta yalipovuja kutoka kwa mabomba ya mafuta ya kampuni ya Shell, yaliharibu ardhi na vyanzo vya maji, katika eneo la Niger Delta, na kuwazuia kulisha familia zao kutokana na athari zake.
Kampuni ya Shell inasema kuwa kuvuja kwa mafuta kulisababishwa na vitendo vya wizi na hujuma na kwamba wamejaribu kusafisha mazingira.
Uamuzi wa mahakama hii leo, huenda ukawa tahadhari kwa makampuni ya kigeni kuwajibikia vitendo vyao katika nchio za kigeni hasa barani Afrika.
Mawakili wanne wa Nigeria, kutoka eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta wanasema kuwa kampuni ya Shell hubuni sera zake kuu katika makao yake makuu mjini Hague na hivyo ni sawa kwa mahakama ya Uhalonzi kusikiliza kesi hiyo.
Ingawa Shell ilikuwa imesisitiza kuwa kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani mwaka 2008,ingepaswa kusikilizwa nchini Nigeria.
Hii bila shaka ni kesi ya kwanza kuhusisha kampuni ya mafuta ya Shell kushtakiwa juu ya madai ya uharibifu wa mazingira

No comments:

Post a Comment