Ndugu wa Msanii
aliyefariki dunia jana, Juma Kilowoko (Sajuki), aliyejitambulisha kwa jina la
Ahmedi Mkotwa, akilia kwa uchungu na kushindwa kuzungumza na waandishi wa habari leo, nyumbani
kwa Sajuki, Tabata jijini Dar es Salaam. "Alinichukua nyumbani akaniambia
mdogo wangu twende ukatafute maisha na kweli tulipanga mambo mengi lakini....",
akashindwa kuendelea kuzungumza. Mazishi ya Msanii huyo yanatarajiwa kufanyika
kesho, siku ya Ijumaa kwenye makaburi ya Kisutu jijini. Wakati huo huo, katika
kile kinachoonekana kuna mpasuko mkubwa ama mgawanyiko miongoni mwa wasanii wa
filamu, kundi kubwa la wasanii hao, ambao kwenye baadhi ya misiba ya wasanii waliokufa
mwaka jana walishuhudiwa wakiwa kwenye suti nyeusi, kwenye msiba huu hadi sasa hawajaonekana
kabisa. Mitandao kadhaa inayofuatilia kwa karibu msibani hapo imeshuhudia hali hiyo, ambayo haikutarajiwa hasa ikizingatiwa marehemu alikuwa mmoja wa wasanii nyota katika tasnia hiyo nchini. Mtandao huu utakuwa kwa karibu kufuatilia matukio mbalimbali na kuyabainisha kila inapobidi. Bayana itafuatilia kujua kulikani hata yakajiri masuala hayo, yaliyoelezwa na wapembuzi wa mambo kuwa siyo ya kiungwana hata kidogo. |
No comments:
Post a Comment