Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa na mkewe, mama Regina Lowassa wakiwapungua mikono wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha mchana alichokiandaa kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2013. Hafla hiyo, ilifanyika nyumbani kwake Monduli.
Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Beatrice Shelukindo (wa pili kulia), akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Andrew Chenge, wakati wakiwasili kwenye hafla ya chakula cha mchana kilichokuwa kimeandaliwa na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha, Papa King na mdau Mathias (MNEC), wakiwasili kwenye hafla hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, akihutubia wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya chakula cha mchana alichokiandaa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013, katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, Monduli.
Wageni waalikwa wakipata chakula nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
No comments:
Post a Comment