TANGAZO


Thursday, January 3, 2013

CUF chatoa taarifa za upotoshwaji madai ya wananchi wa Mtwara


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
PROF.MUHONGO AMEPOTOSHA UKWELI WA MADAI YA WANANACHI WA MTWARA
03/01/2013
CUF-Chama cha Wananchi  Kimesitushwa na tamko la Serikali, lililotolewa na Prof Muhongo kuhusu Maandamano yaliofanywa na Wakazi wa Mtwara, ili kuishinikiza Serikali kuweza kutumia Gesi ilopatikana Mtwara kuweza kujenga Viwanda vitakavyoongeza Ajira kwa watu wa Mtwara.

Serikali imekuja juu na kutoa kauli kwamba Gesi iliopatikana Mtwara ni % 14 na Lindi ni % 7 na %78 inapatikana kwenye Bahari ya kina kirefu na Pwani ni % 1  inapatikana kwenye Bahari ya kina kirefu na kwa hivyo si busara kwa Wakazi wa Mtwara kudai kujengwa kwa Viwanda kwa kutumia Gesi hiyo Hata hivyo Prof Muhongo hakusema hiyo % 78 inayopatikana kwenye kina kierefu cha Bahari kipo kwenye Mkoa gani ?.

CUF – Chama cha Wananchi kinatilia shaka kauli hiyo na kauli nyingine iliosema kwamba, mbona mapato ya Dhahabu na Tanzanite na umeme unaozalishwa na kwenye Mikoa ya Mororogo na Maji ya Ruvu yanatumika maeneo mengine.

Hoja hizi ni dhaifu kwakua, hoja ya watu wa Mtwara, si kuitumia Gesi au mapato yatokanayo na Gesi, Hoja ya watu wa Mtwara ni kwamba, wanaihitaji Serikali kujenga Viwanda vitavyotumia gesi kwenye Mkoa huo ili kuongeza Ajira kwa watu wa Mkoa huo.

CUF- Chama cha Wananchi, kina hoji, kwa nini Kiwanda cha Makaa ya Mawe hakijajengwa Dar es Salaam, kwa nini Usafishaji wa Dhahabu haufanyiki Dar es Salaam na badala yake unafanyika kwenye Maeneo yanapopatikana Dhahabu kama vile Mbeya kwenye Makaa ya Mawe, Mwanza, Arusha,Shinyanga,Geita, Mara na Maeneo mengine.

Watu wa Mtwara wanaendeleza utaratibu ule ule uliosasisiwa na Serikali wa kuacha dhahabu iliogunduliwa kwenye maeneo ya Mwanza,Arusha,Mara,Geita,Shinyanga,Manyara na Makaa ya Mawe pale Mbeya, yaendelee kuchimbwa na kusafishwa kwenye maeneo hayo ili kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo husika.

Hoja ya watu wa Mtwara si kuzuia mapato yatokanayo na Gesi , bali ni kujengewa Viwanda vitavyotumia malighafi ya Gesi ili kuongeza ajira. Hoja ya Watanzania wote kunufaika na Mapato yatokanayo na Mali ya Asili ni hoja sahihi na kamwe haipingwi na watu wa Mtwara, kwani mapato yatatokana na Viwanda Vitavyojengwa hapa Mtwara , pia yataingia kwenye pato la Taifa chini ya Hazina ya Taifa.

Hata kampuni iliopewa tenda ya kutengeneza bomba la kusafirisha Gesi hiyo kuelekea Dar es Salaam, ilitoa ushauri kwa Serikali juu kujenga Kiwanda cha Mbolea kwa kutumia Gesi hiyo , kitaongeza ajira kwa vijana wa Mtwara na Mikoa ya jirani. Lakini ushauri huo , umepuuzwa na Serikali. C

UF – Chama cha Wananchi kinatilia mashaka na tamko hili la Serikali, hatuamini kama tamko hili limeandaliwa na Prof Muhongo, tamko hili limekuwa la kisiasa zaidi, inawezekana tamko hili hali kuandaliwa na mtu makini kama Prof Muhongo.

CUF- Chama cha Wananchi kinatoa wito kwa Serikali juu ya kutimiza ahadi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ya kujengwa kwa Viwanda Mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuongeza ajira kwa wakazi wa Mikoa hiyo. Prof Muhongo anapaswa kukumbuka ahadi iliotolewa na Rais na kusiwe na majibu mepesi kwenye hoja na ahadi ya msingi ilotolewa na Rais.
Imetolewa na
Abdul Kambaya
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma CUF – Taifa
0719 566 567

 

No comments:

Post a Comment