TANGAZO


Sunday, January 6, 2013

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akagua Migodi Same, kuangalia Uchafuzi wa Mazingira

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula akizungumza na wanakijiji cha Marieni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, alipokwenda kukagua Shughuli za Uchafuzi wa  Mazingira katika kjiji hicho leo. (Picha zote Ali Meja)
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula akiangalia madini aina ya Bauxite, yanayochimbwa na Kampuni ya Willy Enterprises, alipokwenda kuangalia hali ya uchafuzi wa Mazingira katika Kijiji cha Marieni, Wilaya Same, mkoani Kilimanjaro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula akizungumza na Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Eng. Benventure Baya na Mkurugenzi wa Mazingira, Ofisi ya Makmu wa Rais, Dk. Julias Ningu na Ofisa Mwandamizi, Timotheo Mande mara baada ya kutembelea uchimbaji wa madini aina ya Bauxite, yanayochimbwa kwenye kijiji cha Marieni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro leo. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akionyeshwa mashine ya Ex-rey kwa ajili ya kupimia madini ya Bauxite na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchimba madini hayo, yanayotumika kutengeneza Saruji, Eng. Alumbwage Mhagama, wakati alipofanya ziara ya kikazi ili kuona hali ya Mazingira kwenye Kijiji cha Marieni Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akiangalia mashine ya Ex-rey, inayotumika kupimia madini ya Bauxite, wakati alipofanya ziara ya kikazi ili kuona hali ya Mazingira kwenye Kijiji cha Marieni Wilaya ya Same, Mkoa wa Kilimanjaro leo. Kushoto kwake ni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchimba madini hayo, Eng. Alumbwage Mhagama

No comments:

Post a Comment