TANGAZO


Saturday, January 5, 2013

Kiir na Bashir waendelea kuzungumza

Marais wa Sudan Kusini na Sudan wanaendelea na mkutano wao kwa siku ya pili mjini Addis Ababa, Ethiopia, ili kujaribu kukwamua juhudi za kurejesha amani kati ya nchi mbili hizo.
 
Al Bashir na Salva Kiir

Muafaka uliofikiwa mwezi wa Septemba baina ya Rais Omar al Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini bado haukutekelezwa.

Mataifa ya magharibi yamezisihi nchi mbili hizo ziondoe majeshi yao haraka kutoka sehemu za mpakani ambayo inakusudiwa kuwa eneo la amani.

Mpatanishi mkuu wa Sudan Kusini, Pagan Amum, alisema Bwana Kiir anazungumza na Bwana Bashir juu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyotiwa saini mwaka jana, yaliyoruhusu mafuta kusafirishwa tena kutoka Sudan Kusini kwa kupitia Sudan, na namna ya kulinda mpaka wenye utatanishi na mapigano pamoja na hatima ya Abyei.

No comments:

Post a Comment