TANGAZO


Thursday, August 16, 2012

Waziri Mwinyi azindua vitabu vya ubora wa huduma za maabara kitabibu

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akikata utepe kuzindua vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili, leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa washirika wa huduma za Afya duniani (CLSI), Connie Adams. (Picha zote na Aron Msigwa –MAELEZO)

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akiowaonesha wadau wa huduma za afya nchini (hawapo pichani), moja ya kitabu cha mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu, kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili wakati alipokuwa akikizindua, Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa washirika wa huduma za Afya duniani (CLSI), Connie Adams (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Magreth Mhando.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu sekta ya afya nchini mara baada ya kuzindua vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara nchini jijini leo.

Viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo,  Dk. Hussein Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka ndani na nje ya nchi leo, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu. 

No comments:

Post a Comment