Askari Polisi akiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya kinondoni wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi akiangalia badhi ya vifaa vilivyokuwemo ndani ya moja ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi, akimuongoza mmoja wa vijana waliokuwa wakiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni leo.
Mmoja wa askari Polisi, akimuongoza kijana mwingine aliyekuwa akiwatishia, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya wazi, Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam kuelekea kwenye gari tayari kwa kuwapeleka kituoni leo.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo lililovamiwa maeneo ya Madale Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Dereva wa gari la Jambo Leo, Privatus Kachema, akiangalia zoezi la uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi maeneo ya Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya nyumba zilizovunjwa katika oparesheni ya uvunjaji wa nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi la Madale leo.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likivunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo hilo la wazi.
Tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, likiendelea kuvunja moja ya vibanda vilivyojengwa kwenye eneo.
Askari Polisi na Mgambo wa Manispaa ya Kinondoni, wakikagua moja ya kibanda kabla ya kuvunjwa na tingatinga la Manispaa hiyo, wakati wa zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi Madale Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.
Askari Polisi na mgambo wa Manispaa ya Kinondoni wakiangalia tingatinga la Manispaa hiyo, wakati likivunja nyumba na vibanda vilivyojengwa kwenye sehemu za wazi zinazodaiwa kuvamiwa isivyo halali na watu ambao walikuwa wakiviuza kwa baadhi ya wananchi wengine maeneo ya Madale wilayani humo.
Askari Polisi wakiangalia mabaki ya kibanda kilichobomolewa na tingatinga la Manispaa ya Kinondoni, wakati walipokuwa wakisimamia zoezi la kuvunja nyumba na vibanda vya wavamizi wa eneo la wazi maeneo ya Madale, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya bango lililokutwa limeandikwa na watu hao, likiwa na ujumbe uliokuwa ukimshutumu Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela na OCD wake.
Mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa wavamizi wa eneo hilo, aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Said, akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kupata athari kichwani wakati alipokuwa akiwekwa chini ya ulinzi na askari Polisi kwenye maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment