
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Amos Makala (katikati), akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa (kulia) na Mkuu wa Chuo cha Mipango Dodoma, Constantine Lifurilo, wakifuatilia zoezi la ufunguaji wa semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi waandamizi kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, mwezi Okotba nchini kote. Mafunzo hayo yalifunguliwa leo, ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Chuo cha Mipango Dodoma
Wahariri na waandishi waandamizi wakifuatilia mafunzo wakati wa semina yao ya siku tatu kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, mwezi Okotba nchini kote. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo, ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Chuo cha Mipango mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo, Amos Makala.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Amos Makala akifungua semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi waandamizi wa habari, kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inayotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, mwezi Okotba nchini kote. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo, ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Chuo cha Mipango Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makala akifungua semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi waandamizi wa habari kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 inayotarajia kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, mwezi Okotba nchini kote.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makala (wa pili kulia), akiagana na Viongozi mbalimbali wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mara baada ya kuifungua semina ya siku tatu ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali leo, Chuo cha Mipango mjini Dodoma. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa (wa pili kushoto), Afisa Uhamasishaji wa Sensa wa NBS, Said Ameir (kushoto) na kulia ni Mkuu wa chuo cha Mipango - Dodoma, Constantine Lifuliro.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Amos Makala (wa tatu kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya wahahriri wa vyombo vya habari vya hapa nchini leo, Chuo cha Mipango mjini Dodoma mara baada ya kuifungua semina ya siku tatu kwa wahariri na waandishi hao, kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inayotarajiwa kufanyika usiku wa kuamkia tarehe 26, mwezi Okotba nchini kote.
No comments:
Post a Comment