TANGAZO


Saturday, July 14, 2012

Wabunge Kamati ya Huduma za Jamii waelimisha kuhusu Bima ya Afya

 Ofisa Nyaraka wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Erastus Msigwa akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, jinsi wanavyohifadhi kwa njia ya kisasa kadi za wananchama wa mfuko huo, wakati wa wa semina waliyoandaliwa wabunge hao leo, Makao Makuu ya NHIF, Dar es Salaam. 
Ofisa Nyaraka wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Erastus Msigwa akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, moja ya mafaili ya wananchama yanayohifadhiwa kwa njia ya kisasa kadi za wananchama wa mfuko huo, wakati wa wa semina waliyoandaliwa wabunge leo katika Makao Makuu ya NHIF, Dar es Salaam. 
 Meneja Idara ya Uanachama wa NHIF, Ellentruder Mbogoro, akitoa maelezo kwa wabunge jinsi wanavyohifadhi mafaili ya wana chama kwa njia ya kisasa
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akifafanua jambo kwa wabunge wa kamati hiyo, wakati wa semina yao hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba (kushoto), akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi pamoja na Naibu wake, Dk. Seif , ambao pia walihudhuria semina hiyo.(Picha zote na Richard mwaikenda)

No comments:

Post a Comment