TANGAZO


Sunday, July 15, 2012

Viongozi Wizara ya Afya wakutana na Ujumbe wa Biashara na Uwekezaji Huduma za Afya wa Netherland

Kaimu Mgaga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando, akizungumza na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland  mara baada ya ujumbe huo kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Afya na Ustawi  wa Jamii, jijini Dar es Salaam jana.



Kaimu Mgaga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando (kushoto), akizungumza na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland, jijini Dar es Salaam jana.


Kamishina wa Idara ya Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya, Danford Makala (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Ustawi wa Jamii wakati wa mkutano  kati ya Ujumbe  wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland na watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dar es Salaam jana.


Meneja Mkuu na Mmiliki wa Hospitali zinazojengwa kwa kutumia makontena (Hospitainer) na kuweza kupelekwa kutoa huduma  za afya maeneo yoyote  kutoka nchini Netherland, Rolof Mulder, akiongea na Watendaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakati akielezea namna Kampuni hiyo inavyofanya kazi zake.


Baadhi ya viongozi wa Ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland, wakifuatilia fafanuzi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na watendaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dar es Salaam jana.


Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Biashara na Uwekezaji katika huduma za afya kutoka nchini Netherland. (Picha na Aron Msigwa -MAELEZO)

No comments:

Post a Comment