TANGAZO


Sunday, July 15, 2012

Mkutano wa Uchaguzi Yanga, Diamond Jubilee Dar es Salaam

Baadhi ya wanachama wa Yanga, wakiingia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi mbalimbali za uongozi za klabu hiyo, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya wanachama wa Yanga, wakijiorodhesha ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi mbalimbali za uongozi za klabu hiyo, Dar es Salaam leo.

 Baadhi ya wahudumu kwenye mkutano huo wa kujaza nafasi mbalimbali za uongozi wakiwa wamepunzika wakisubiri kutoa huduma wakati wa mkutano huo leo, Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wa Yanga, wakiomba dua kwa ajili ya kuombea amani uchaguzi wao, kabla ya mkuato huo wa uchaguzi kuanza rasmi leo, Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Wanachama wa Yanga, wakiomba dua kwa ajili ya kuombea amani uchaguzi wao, kabla ya mkuato huo wa uchaguzi kuanza rasmi leo, Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wagombea wa Yanga, wakiomba dua kwa ajili ya kuombea amani uchaguzi wao, kabla ya mkuato huo wa uchaguzi kuanza rasmi leo, Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa, akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi mbalimbali za uongozi zilizokuwa wazi. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji mstaafu, John Mkwawa.

 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, ambao ni wadhamini wa vilabu na Ligi Kuu nchini, George Kavishe, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji mstaafu, John Mkwawa na kulia ni  Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji mstaafu, John Mkwawa , akizungumza na kutoa ufafanuzi kuhusu hatua mbalimbali za uchaguzi huo, utakavyoendeshwa hadi kuwapata viongozi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu hiyo.Kulia ni Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa na katikati ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, ambao ni wadhamini wa vilabu na Ligi Kuu nchini, George Kavishe.

Mmoja wa waliokuwa wachezaji wa Yanga, Ally Mayayi akiteta jambo na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, katika uongozi uliopita Davies Mosha.

 Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), Deogratius Lyatoo, akizungunza katika uchaguzi huo na kuitakia klabu hiyo uchaguzi wenye mafanikio.
z
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa kwenye mkutano huo wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizowazi wakifuatilia matukio mbalimbali.

Mmoja wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti, Yussuf Manji akiwa na mmoja wa wagombea wa nafasi za ujumbe, Abdallah Bin Kleb kwenye mkutano huo.

Mmoja wa wagombea wa nafasi ya Uenyekiti, Yussuf Manji akiwa na miongoni mwa wagombea wa nafasi za ujumbe, Abdallah Bin Kleb na Yono Kavela kwenye mkutano huo.

Wanachama wa Yanga, wakisikiliza maelezo mbalimbali ya wagombea wakati wa mkutano wa uchaguzi mdogo wa uongozi wa timu hiyo, ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment