Miss Sinza 2012, Brigita Alfred (katikati), akipunga mkono kwa furaha
wakati akiwa na washindi wenzake, mshindi wa pili Judith Sangu
(kushoto) na watatu Esther Mussa, baada ya kutangazwa washindi katika
shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa
Mawela Social, Sinza Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya SPM-Sufiani Photo Magic na Mtandao wa
Sufianimafoto.blogspot.com, Nasma Sufiani, akimvisha taji na kumkabidhi
zawadi Maria John, baada ya kuibuka kidedea katika shindano la kumska
Sufianimafoto Miss Talent, lililofanyika ndano ya shindano hilo la Miss
Sinza katika Ukumbi wa Mawela Social, Sinza jijini Dar es Salaam.
Sufianimafoto Miss Talent, Maria John, akiwa na furaha baada ya kuvishwa taji hilo na kukabidhiwa zawadi yake.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia)
akiwa na baadhi ya wanakamati wakishuhudia shindano hilo.
Mshiriki, Nancy, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
![]() |
Mshiriki,Naima mohamed, akipita jukwaani na vazi la ufukweni. |
Mshiriki, Maria John, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
Msanii wa Vichekesho, ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Uongo
Kweli, akishambulia jukwaa, wakati wa onyesho hilo na kuwapagawisha
vilivyo, mashabiki wa fani ya urembo waliokuwapo ukumbini hapo.
Mshiriki, Mariam Miraji, akipita jukwaani na vazi la ufukweni.
Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia shindano hilo.
Madj wa Sufianimafo, wakiwa katika mitambo ya Sufianimafoto, iliyokuwa
ikitumika katika shindano hilo, wakiendesha shughuli nzima ukumbini
hapo.
Pozi la Masawe Mtata, kabla hajapanda jukwaani, huku akiwa ameketi na
wanadada ambao baada ya kushuka jukwaani walianza kumgombea, ''he kumbe
tumekaa na Masawe hapa hatujui, hebu nipe namba yako'', wasilikika
madada hao wakisema kila mmoja akiomba namba huku mwingine akisikika
kumpiga mkwara Masawe, ''Ole wako umpe namba huyo mdada ntakupasua''
alsema mdada mmoja kati ya hawa walionyuma yake kana kwamba yeye
alikuwa tayari amekwisha wini kupata namba.
Waimbaji wa Twanga Pepeta, wakishambulia jukwaa.
Wanenguani na waimbaji wa Twanga, wakishambulia jukwaa. (Picha zote na Muhidini Sufiani wa Sufianimafoto.blogspot)
No comments:
Post a Comment