Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu' (katikati), akiandika kero za wapiga kura wake wa mtaa wa Mafuriko, Bungoni Ilala, wakati alipowatembelea na kukutana nao kwa ajili ya kuwasikiliza kero wanazokabiliana nazo mtaani hapo leo.
Mwananchi Frank Mmari, akimuelezea Mbunge Zungu (hayupo pichani) moja ya kero wanazokabiliana nazo kwenye mtaa huo wa Mafuriko, Bungoni Ilala, wakati alipowatembelea na kusikiliza kero zao leo asubuhi mtaani hapo.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akisisitiza jambo kwa wapiga kura wake wa mtaa wa Mafuriko, Bungoni Ilala, wakati alipowatembelea kwa ajili ya kuwasikiliza kero wanazokabiliana nazo mtaani hapo leo.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wapiga kura wake wa mtaa wa Mafuriko, Bungoni Ilala, wakati wa mkutano wake wake wa kuwasikiliza kero zao wanazokabiliana nazo mtaani hapo.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wapiga kura wake wa mtaa wa Mafuriko, Bungoni Ilala, wakati alipokuwa akijibu baadhi ya hoja walizokuwa wakitaka ufafanuzi kwake kwenye mkutano wake wake huo leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Shina la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mtaa wa Mafuriko, Bungoni Ilala jijini Dar es Salaam, Mtakwisha Ally, akimweleza Mbunge Zungu moja ya kero za mtaa huo, ambapo aliitaja kero kubwa kuwa ni takataka ambazo huingia kwenye mfereji mkubwa wa kupitishia maji taka kutoka barabara ya Nyerere hadi Msimbazi, unaopita kwenye mtaa huo.
Katibu wa CCM, tawi la Bungoni, Fatuma Rajab, akitoa ufafanuzi kwa wananchi wakazi wa mtaa huo, wakati alipotakiwa na Mbunge Zungu (katikati), kufanya hivyo kutokana na hoja zilizokuwa zikitolewa na wakazi hao kwa Mbunge wao huyo, alipowatembelea leo asubuhi kwa ajili ya kutaka kujua kero wanazokabiliana nazo.
Katibu wa CCM, tawi la Bungoni, Fatuma Rajab, akisisitiza jambo wakati akitoa ufafanuzi huo kwa wananchi wakazi wa mtaa huo, mbele ya Mbunge wao huyo, Mussa Zungu (katikati), leo asubuhi, alipowatembelea kwa ajili ya kutaka kujua kero wanazokabiliana nazo.
Baadhi ya wakazi wa mtaa huo, wakisikiliza kwa makini majibu ya hoja zao yaliyokuwa yakitolewa na Katibu huyo wa Tawi la Bungoni, Fatuma Rajab baada ya kutakiwa na Mbunge Zungu kufanya hivyo kwenye mkutano wake huo na wapiga kura wake hao.
No comments:
Post a Comment