TANGAZO


Sunday, July 15, 2012

Simba kama Yanga, yachapwa bakora 2 kavu na URA ya Uganda

Mchezaji Ssenkoomi Samuel wa URA ya Uganda akiutuliza mpira huku nyuma yake akifuatwa na Danny Mrwanda wa Simba, wakati wa mchezo wa Klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kagame CECAFA Cup), Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-0. (Picha na Kassim Mbarouk)


Mchezaji Ssenkoomi Samuel (kulia) wa URA ya Uganda na Danny Mrwanda wa Simba wakiwania mpira wakati wa mchezo huo leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


 Mashabiki wa Simba ya Tanzania, wakifuatilia mchezo kati ya timu yao na URA ya Uganda, ambapo 
Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-0, mbele ya wababe hao wa Uganda.


 Felix Sunzu wa Simba (kushoto), akijaribu kumpiga chenga Munaaba Allan wa URA, wakati wa kipute hicho.


 Hadi mwisho wa mchezo, ubao wa matokeo ulikuwa ukionesha URA (Uganda) 2, Simba (Tanzania) 0.


 Mashabiki wachache wa Yanga, waliojitokeza kwenye mchezo huo, wakishangilia matokeo hao ili kuwakejeli watani zao, Simba kwani nao walipata kipigo kama hicho kutoka kwa Atletico ya Burundi jana.


Mchezaji Danny Mrwanda wa Simba (kushoto), akiwania mpira na Ssenkoomi Samuel wa URA ya Uganda wakati wa mchezo huo leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi ‘Bobani’ akimiliki mpira mbele ya beki wa URA ya Uganda, Ssenkoomi Samuel katika mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni.
 Wachezaji wa Simba wakibadilishana mawazo wakati wakitoka mapumziko.
Mchezaji Juma Nyosso wa Simba (kulia), akipambana na Ssenkoomi Samuel wa URA ya Uganda katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment