TANGAZO


Monday, July 9, 2012

Tanesco yagundua wizi wa umeme, Mkurugenzi aendesha zoezi la kukata umeme wa wizi

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando (katikati), akimuhoji Meneja wa baa (kushoto) ya King Palace ya Keko jijini Dar es Salaam leo kwa tuhuma za wizi wa umeme ambao alikua anaufanya kwenye baa hiyo na kuwaamuru Polisi wa mchukulie hatua za kisheria ambapo Polisi walimchukua na kuondoka naye. Zoezi la kuwasaka wezi wa umeme limeshika kasi baada ya kukamatwa kwa watu watano wanaotuhumiwa kuiba umeme kwa njia ya mtandao.
Mtaalamu wa mifumo ya Umeme wa Tanesco (kulia) akimhoji Msimamizi wa baa ya Miami Shambwe (kushoto) ya Keko jijini Dar es Salaam baada ya mita ya umeme wa baa hiyo kukutwa imechezewa huku Mkurugenzi wa Shirika hilo William Mhando (katikati) akishuhudia.
Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando, akitoa amri umeme ukatwe mara moja kwa mtu aliyejiunganishia nishati hiyo. (Picha na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment