TANGAZO


Monday, July 9, 2012

Yatima aishiye mazingira magumu aongoza mtihani wa muhula darasa la saba

 Mwenyekiti wa Kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha New Hope Family, Omar Rajab (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mmoja wa watoto wa kituo hicho, Joel Joseph (hayupo pichani), alivyofanya vizuri kwenye mtihani wake wa kumaliza muhula na kushika nafasi ya kwanza darasa la saba katika shule ya Msingi Ungindoni, wilayani Temeke. Wengine ni Mlezi wa kituo hicho, Mariam Pius(kushoto) na kulia ni Katibu wa kituo hicho, Hashim Yusuf Mahmoud. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Mlezi Mariam Pius, akitayarisha koja kwa ajili ya kuvisha mwanafunzi aliyefanya vizuri kwenye mitihani yake ya muhula, anayelelewa na kitu hicho, Joel Joseph (katikati), wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo. Kulia ni Mshauri wa kituo hicho, Michael Gumbo.

Mlezi Mariam Pius, akimaliza kuvisha koja mwanafunzi aliyefanya vizuri kwenye mitihani yake ya muhula, anayelelewa na kitu hicho, Joel Joseph (katikati), wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mshauri wa kituo hicho, Michael Gumbo.

Mshauri wa kituo hicho, Michael Gumbo, akimkabidhi zawadi za vitabu na madaftari, mwanafunzi Joel Joseph wa Shule ya Msingi Ungindoni wilayani Temeke anayelelewa katika kituo cha New hope Family, wakati wa hafla ya kumpongeza na kumtunza iliyofanyika Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo. Wengine ni kushoto ni Mlezi kituo, Mariam Pius na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kituo, Omar Rajab.

 Mshauri wa kituo hicho, Michael Gumbo, akimkabidhi kadi ya kumpongeza mwanafunzi Joel Joseph wa Shule ya Msingi Ungindoni wilayani Temeke anayelelewa na kituo cha New hope Family, ili kumtia moyo na kuwapa hamasa wenzake katika changamoto ya kufanya vizuri kwenye masomo yao wakati wa hafla ya kumpongeza na kumtunza iliyofanyika Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo. Wengine ni kushoto ni Mwenyekiti wa kituo hicho, Omar Rajab na kulia ni Katibu wake,
Hashim Yusuf Mahmoud.

 Mshauri wa kituo cha Kulelea watoto waishio katika Mazingira Magumu cha New Hope Michael Gumbo, akiwaonyesha waandishi wa habari kadi aliyoinunua kwa ajili ya kumkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba, Joel Joseph wa Shule ya Msingi Ungindoni wilayani Temeke, anayelelewa katika kituo hicho, baada ya kufanya vizuri katika mtihani wake wa kumaliza muhula licha ya kuishi katika mazingira magumu. Wengine kushoto ni mlezi wa kituo hicho, Mariam Pius na Mwenyekiti wa Kituo Omar Rajab.

 Mwanafunzi Joel Joseph wa Shule ya Msingi Ungindoni wilayani Temeke, anayelelewa katika kituo cha New Hope Family, akitoa shukurani kwa viongozi wa kituo hicho kutokana na zawadi walizompatia na kuahidi kuongeza bidii zaidi katika masomo yake. Kutoa kushoto ni mlezi wa kituo hicho, Mariam Pius, Mwenyekiti wa kituo, Omar Rajab na Katibu wake, Hashim Yusuf Mahmoud.

Katibu wa kituo watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha New Hope Familia Hashim Yusuf Mahmoud, akizungumza katika kuwashukuru waandishi na watu mbalimbali wanaojitolea kuwasaidia katika kikiendesha kituo chao hicho na kuwataka kutochoka katika kulitekeleza hilo kwani alisema huo ni wajibu wa kila mmoja wetu na sio kwa watu maalum tu.

No comments:

Post a Comment