Makamau wa Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe (katikati),
akiangalia moja ya makaburi ya wapigania Uhuru (ANC), eneo la Mazimbu, mjini Morogoro jana.
Makamu
wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, Julai 9, mwaka huu
alifanya ziara ya siku moja Mjini Morogoro, ililiyokuwa mahusisi kwa
ajili ya kutembelea eneo la Mazimbu, iliyokuwa kambi ya wapingania uhuru
wa Chama cha ANC.
Ziara
hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 20 tangu harakati za
ukombozi wa Afrika Kusini zilipomalizika, katika Kambi hiyo, ANC
iliacha majengo na vitu mbalimbali vilivyokabidhiwa Serikali ya
Tanzania, pia yapo makaburi kadhaa walimozikwa mashujaa hao, ambapo
Makamu huyo wa Rais aliweza kuzuru na kuweka shada la maua katika
mnara wa kumbukumbu ya wapigania uhuru hao pamoja na kupanda mti.
Kabla
ya kufanya shughuli hiyo,alipata fursa ya kutembezwa maneo
mbalimbali yakiwemo majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wapigania uhuru
hao, ikiwemo Shule ya Msingi na Awali, Shamba la Mifuko, Kiwanda cha
samani pamoja na Hospitali .
Makamau wa Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe, akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua kwenye moja ya makaburi ya wapigania Uhuru wa ANC, eneo la Mazimbu mjini Morogoro.
Makamau wa Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe, akipanda mti eneo la Makaburi ya Wapigania Uhuru wa ANC, Mazimbu mjini Morogoro jana.
Makamau wa Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe, akitoka kutembelea hospitali ya Mazimbu, ambayo ilikuwa ikitumiwa na wapigania Uhuru wa ANC, ambapo kwa sasa imekarabatiwa na kuongezwa majengo mapya.
Baadhi ya raia wa Afrika Kusini walioambatana na Makamu wa Rais wa nchi hiyo hapa nchini jana.
Burudani kwa mgeni rasmi, Makamau wa Rais wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe, alipotembelea Shule ya Msingi ya Chief Albert , Mazimbu mjini Morogoro jana. (Picha zote na mdau wetu)
No comments:
Post a Comment