TANGAZO


Saturday, February 18, 2012

Yanga yalazimishwa sare Nyumbani

 Mchezaji Nadir Haroub 'Canavaro' wa Yanga, akimkata kwanja Sabry El Sayed wa Zamalek ya Misri, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zilifungana bao 1-1. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Hamis Kiiza wa Yanga, akijaribu kumpiga chenga Mohamed AbdelShafii wa Zamalek katika mchezo huo. Kulia ni Shadrack Nsajigwa akiwa tayari kutoa msaada.


 Sabry El Sayed wa Zamalek, akipiga mpira krosi mbele ya Omega Seme wa Yanga katika mchezo huo.


 Mohammed AbdelShafii wa Zamalek (kulia), akitafuta mbinu ya kumtoka Shadrack Nsajigwa wa Yanga.


 Haruna Niyozima wa Yanga, akimtoka Hazem Mohamed wa Zamalek katika mchezo huo.


 Mashabiki wa Simba, wakiwashangilia Zamalek ya Misri, wakati waliposawazisha bao katika mchezo huo.


 Mashabiki waliochanganyika wa Yanga na Simba (juu), wakiishangilia Zamalek wakati waliposawazisha bao, huku wenzao wa Yanga, wakiuchuna.


 Shabiki wa Yanga, akiondolewa na askari Polisi kwenye jukwaa walililokuwa wamekaa mashabiki wa Simba katika mchezo huo.


 Hamis Kiiza wa Yanga, akijaribu kumtoka Ahmed Samirosman wa Zamalek katika mchezo huo.


 Haruna Niyozima wa Yanga (kulia), akijaribu kumzuia Ahmed Samirosman wa Zamalek.



Kocha Mkuu wa timu ya Zamalek, Hassan Shehata, akizungumza na Farouk Karim (kulia) wa Nipashe, Muga wa Dutche Welle na John Solombi wa BBC mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, ulioishia kwa sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment