TANGAZO


Saturday, February 18, 2012

CUF kutokushiriki Uchaguzi mdogo wa Arumeru

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kutoshiriki uchaguzi mdogo wa marudio, Jimbo la Arumeru na kudai kuwa ni kutokana na kawaida yao kwa Majimbo yote ya Bara, kila wanaposhika nafasi ya tatu kutoshiriki katika uchaguzi wa marudio kwenye Jimbo husika. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Haki za Binadamu, Amina Mwindau na kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Shaweji Mketo. (Picha na Kassim Mbarouk)


Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu zira ya Kanda ya Ziwa ya kuimarisha Chama, itakayofanywa na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Julius Mtatiro (katikati), Februari 23, 2012. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Haki za Binadamu, Amina Mwindau. (Picha na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment