TANGAZO


Saturday, February 18, 2012

Rais Kikwete, aongoza matembezi ya Vodacom, kuchangia ujenzi Hospitali ya Akinamama na watoto ya CCBRT

 Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Willibroad Slaa (kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali hiyo, Erwin Telemans (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili kulia) na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, wakifanya mazoezi kabla ya matembezi ya kuchangia ujenzi wa Hospitali ya akinamama na watoto ya CCBRT, itakayojulikana kwa jina la
Baobab Hospitali. (Picha na Kassim Mbarouk)


Wakurugenzi na Maofisa wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, CCBRT na wageni waalikwa wakifanya mazoezi kabla ya kuanza matembezi yalioanzia Hoteli ya Golden Tulip na kumalizikia Hospitali ya CCBRT leo asubuhi.

 Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Willibroad Slaa, kabla ya kuanza matembezi ya kuchangia kujengwa Hospitali ya Mama na watoto, (CCBRT).


 Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Willibroad Slaa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Rene Meza, kabla ya kuanza matembezi hayo.


 Rais Jakaya Kikwete, akikatata utepe, ikiwa ni ishara ya kuanza uzinduzi wa matembezi ya kuchangia ujenzi wa Hospitali ya akinamama na watoto, matembezi yaliyojulikana kwa jina la Find your moyo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza na Mwenyekiti wa Bodi ya Hopsitali ya CCBRT, Dk. Willibroad Slaa.


 Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, wakati wa matembezi hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk. Willibroad Slaa na kushoto wanaozungumza ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (wa tatu) na Mkurugenzi wa Vodafone Foundation, Adrew Dunnett na wa kwanza kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom, Mwamvita Makamba.


 Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika Hopsitali ya CCBRT, wakipiga makofi wakati wa Kumpokea Rais Jakaya Kikwete, alipofika hapo kuangalia masuala mbalimbali hospitalini hapo
wakati wa matembezi hayo.


 Rais Kikwete, akisalimiana na wanaushirika wa Mabinti Centre, waliokuwepo kwenye Hospitali hiyo, wakati wa kumalizika kwa matembezi hayo.


 Rais Kikwete, akizungumza na wadau pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki na kuchangia matembezi hayo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.


 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda (kushoto), akimweleza jambo Rais Jakaya Kikwete, wkati wa kumalizika kwa matembezi hao.


 Rais Jakaya Kikwete, akimpatia cheti cha kutambua mchango wao, mmoja wa wafadhili waliotoa zaidi ya sh. milioni tano katika kuchangia ujenzi huo.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya CCBRT, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, wakati alipokuwa akizunguza mara baada ya kumalizika matembezi hayo.


 Rais Jakaya Kikwete, akimweleza jambo Mwenyekit wa Bodi ya Hospitali ya CCBRT, Dk.
Willibroad Slaa (kushoto), wakati walipokwenda kutembelea ujenzi wa hopsitali
hiyo na kuangalia mbuyo, uliokuwepo maeneo hayo hadi hospitali hiyo kupewa jina lake.


Baadhi ya wafanyakazi wa Kitengo cha Mahusiano cha Vodacom Tanzania, wakipozi kwa picha mara baada ya kumalizika kwa matembezi hayo.

No comments:

Post a Comment