Wasanii wakiwa pamoja na waandishi wa habari, wakielekea sehemu zilikojengwa nyumba tano za wasanii, katika kijiji cha Mwazenga/Kimbili Mkuranga mkoani Pwani, leo mchana. Katikati ni msanii, Ahmed Ulotu 'Mzee Chilo'. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania, Cassim Taalib (kulia), Katibu wa Shirikisho hilo, Suleiman Pembe (kushoto), wakiwa na mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki' (wa pili kushoto) na msanii Ahmed Ulotu 'Mzee Chilo', wakitembelea eneo lenye nyumba za wasanii, kijiji cha Mwanzega/Kimbili, Mkuranga, kuangalia maendeleo ya ujenzi wake, wakati walipokwenda kuwatembeza waandishi wa habari ili kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo, leo mchana.
Mzee Chilo (kushoto), akiangalia moja ya nyumba tano, za awali zilizojengwa kwa ajili ya wasanii kijijini hapo. Kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Cassim Taalib.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wasanii Tanzania, Cassim Taalib, akizungumza wa waandishi wa habari, kwenye ujenzi wa nyumba za wasanii, kijiji cha Mwanzega/Kimbili, Mkuranga mkoani Pwani, wakati walipowatembeza waandishi wa habari, kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo leo mchana. Kushoto ni Mwanamuziki Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki, wa kwanza kulia ni msanii Ahmed Ulotu 'Mzee Chilo' na Katibu wa Shirikisho hilo, Suleiman Pembe.
Nyumba za wasanii, zinavyoonekana kijijini hapo kwa sasa, ili kupata nyumba hizo kila msanii, anatskiwa kulipa kiasi cha sh. milioni 7.
Mchungaji Mkwawa Emmanuel wa Kanisa la Evangetical Brotherhood, Ilala jijini Dar es Salaam, akiombea ujenzi wa nyumba hizo katika matembezi hayo.
Sheikh Majaliwa Suleiman, akiomba dua, akimwakilisha Sheikh wa Mkoa, Alihadi Mussa, katika eneo la ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment