Rais Kikwete, akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye meza kuu kabla ya kuanza kikao mjini Dodoma leo. (Picha na Ikulu)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye meza kuu, baada ya kuwasili ukumbini kuzungumza na wabunge wa CCM katika kikao chake na wabunge hao kilichofanyika jana jioni Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.Wengine kutoka kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda, Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, na baadhi ya viongozi wakuu wa Chama hicho, wakiimba wimbo wa hamasa kabla ya kuanza kwa kikao chao, jana jioni, mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa na Katibu Mkuu Wilson Mkama wakimsikiliza Mwenyekiti ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama, akiongea kabla ya kikao kuanza'
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wabunge wa CCM, katika kikao chake na wabunge hao jana katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa.
Mbunge wa Simanjoro Ole Sendeka akitoa hoja zake katika kikao hicho.
Pia Said Mkubwa, akazungumza kwa kina kutoa mchango wake katika kikao hicho na Rais Jakaya KIkwete ili kuboresha mambo.
Baadhi ya Wajunbe wakibadilishana mawazo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijadili jambo kwenye kikao hicho na Rais Jakaya Kikwete, (hayupo pichani) jana jioni.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa wabunge na Rais Jakaya Kikwete, wakimsikiliza Mwenyekiti huyo, wakati alipokuwa akizungumza nao.
Baadhi ya Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakimsikiliza Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati wa kikao hicho.
Wabunge wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo, White House, mjini Dodoma juzi.
Wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakimsikilza Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete kwenye kikao hicho. (Picha na IKULU)
No comments:
Post a Comment