Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Vodacom Tazania, Hassan Saleh, akizungumza wakati hafla ya uzinduzi wa punguzo la gharama la huduma ya M Pesa, kwenye viwanja wa Mlimani City kabla ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda mitaani kwa ajili ya promosheni hiyo, leo asubuhi jijini Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)
|
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wakiwa kwenye Viwanja vya Mlimani City, Makao Makuu ya Kampuni hiyo, wakati wa uzinduzi wa punguzo la asilimia 25 la gharama la huduma ya M Pesa, leo jijini Dar es Salaam.
|
Mkuu wa Kitengo cha Udhamini wa Vodacom, George Rwehumbiza (kushoto) na Meneja Mauzo wa M Pesa, Henry Tzamburakis, wakionesha vipeperushi, wakati alipokuwa akielezea kuhusu kununua muda wa maongezi kwa M Pesa na kupata nyongeza ya asilimia 25 pamoja na cha Tuma pesa kwa M pesa kwa gharama kuanzia sh. 50, iliyozinduliwa, leo Makao Makuu ya kampuni hiyo, Mlimani City na Mkurugenzi Mkuu, Rene Meza.
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa punguzo la gharama la huduma ya M Pesa, kwenye viwanja wa Mlimani City kabla ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda mitaani kwa ajili ya promosheni hiyo, leo asubuhi jijini Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)
|
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Makao Makuu ya Vodacom, Viwanja wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza, akipunga bendera ya Vodacom, ili kuruhusu magari kuondoka kuelekea mitaani kwa ajili ya promosheni hiyo.
Afisa Utawala Kitengo cha Biashara, Godfrey Mbowe, akibandika kipeperushi cha M Pesa kwenye kibanda cha mfanyabiashara ndogondogo, Gongo la Mboto, wakati wa Promosheni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom, wakiwaeleza wafanyabiashara wa duka la dawa la Bahari, Gongo la Mboto, kuhusu punguzo la gharama la huduma ya M Pesa, wakati wa promosheni hiyo.
|
Mmoja wa Maofisa wa Vodacom Tanzania, Jacque Veermak, aliyekuwemo kwenye msafara wa Gongo la Mboto, akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa kundi hilo kabla ya kuingia mitaani kuelezea punguzo hilo katika promosheni hiyo.
|
Mkuu wa msafara, uliokwenda Gongo la Mboto, Allen Njumbo, akimpongeza mteja mpya wa Vodacom, aliyejiunga na huduma ya M Pesa, Rabia Mohammed, baada ya kumpatia zawadi ya fulana ya promosheni ya punguzo la gharama kwa asilimia 25 la huduma hiyo.
|
Mkuu wa msafara wa promosheni ya punguzo la gharama la M Pesa, uliokwenda Gongo la Mboto, akiwapatia maelezo juu ya vipeperushi vya usalama, wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, waliokuwa kwenye msafara wake huo.
|
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wakizirudi ngoma wakati wa promosheni hiyo.
No comments:
Post a Comment