TANGAZO


Wednesday, February 15, 2012

Viingilio mchezo wa Yanga, Zamalek vyatajwa

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, akitangaza viingilio vya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zamalek ya Misri, mchezo utakaochezwa Jumamosi hii, Uwanja wa Taifa, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Prime Time Promotion, Balozi Kindamba, wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya timu hiyo, Mohamed Bhinda. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine, akizungumza katika mkutano huo, kuelezea kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya timu yao, pia wachezaji walio majeruhi, ambao hawatokuwemo kwenye timu hiyo, siku ya mchezo huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya RAYS (T), Prasanna Kumar.


 Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Prime Time Promotion, Balozi Kindamba, akionesha tiketi na kifaa cha kusomea tiketi hizo, ambacho kitatumika kutambua tiketi halali na zile zilizokwisha kutumika pia kutoa hesabu halisi za jumla ya watazamaji watakaoingia kwenye mchezo huo.

No comments:

Post a Comment