TANGAZO


Saturday, February 25, 2012

Tanzania kunufaika na Elimu kwa njia ya simu na komputa

 Mtaalam wa matumizi ya teknolojia ya simu katika utoaji wa elimu kutoka Chuo Kikuu cha Stanford,  Calfonia nchini Marekani Dk. Paul Kim, akitoa ufafanuzi kwa wadau wa Elimu na Mawasiliano, kuhusu ufanisi wa maendeleo ya teknolojia ya simu katika utoaji wa elimu duniani na namna Tanzania inavyoweza kufaidika na teknolojia hiyo katika suala. Elimu  kuanzia ngazi ya msingi mpaka Vyuo Vikuu,  Dar es salaam leo Februari 25, 2012. (Picha na Aron Msigwa - Maelezo)

 Kamishina wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Benjamini Kulwa akizungumza na wadau wa Elimu na Mawasiliano, wakati akifungua mkutano uliojadili umuhimu wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika utoaji wa elimu jijini Dar es salaam leo.

 Mtaalamu wa Elimu na Mafunzo, Zamaradi Saidi, akitoa utangulizi kwa washiriki waliohudhuria mkutano wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya simu katika utoaji wa elimu jijini leo.




Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya mawasiliano katika utoaji wa elimu kwa kutumia simu, wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment