TANGAZO


Wednesday, February 29, 2012

Taifa Stars, Msumbiji zatoshana nguvu

 Golikipa wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Juma Kaseja, akiruka juu ili kuuchukua mpira uliorudishwa kwa kichwa na Juma Nyosso (mbele yake), wakati timua hiyo, ilipocheza na Msumbiji, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Februari 29, 2012, katika micuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Afrika (AFCON 2013), Afrika ya Kusini. Timu hizo zimetoka suluhu kwa kufungana bao 1-1. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Mashabiki wa timu ya Msumbiji wakionesha kitambaa chenye jina la nchi yao, wakati wa mchezo huo.


 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars), wakielezana jambo wakati timu hiyo, iliporudi uwanjani kuendelea na kipindi cha pili leo jioni katika mpambano huo.


 Mchezaji wa timu ya Taifa Stars, Vicent Barnabas (kushoto), akipambana na Elias Pelembe wa Msumbiji katika mchezo huo


 Mchezaji wa timu ya Taifa Stars, Vicent Barnabas (kushoto), akipambana na Clesio Bauque wa Msumbiji katika mchezo huo.


 Mchezaji wa timu ya Taifa Stars, Aggrey Morris (kushoto), akipambana na Elias Pelembe wa Msumbiji katika mchezo huo

 Mashabiki wa Msumbiji, wakifuatilia timu yao wakati ilipocheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.


 Eduado Jumise wa Msumbiji, akimweleza jambo kocha wake wa timu ya timu hiyo, Engle Gert, baada ya kutakiwa kurudi Uwanjani kucheza ngwe ya mwisho ya mchezo huo, leo jijini.


 Eduado Jumise wa Msumbiji, akimweleza jambo kocha wake,  Engle Gert wa timu hiyo, baada ya kutakiwa kurudi Uwanjani kucheza ngwe ya mwisho ya mchezo huo, leo jioni.


 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Msumbiji (Black Mamba), wakiingia uwanjani kwa ajili ya kumalizia ngwe ya Pili ya mchezo wao, kati ya timu hiyo na Taifa Stars ya Tanzania, Dar es Salaam leo jioni.

Waamuzi wa mchezo kati ya timu ya Taifa Stars na Msumbiji wakiingia Uwanjani kwa ajili ya kuanza ngwe ya pili ya mchezo huo, leo jioni jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka suluhu ya kufungana bao 1 kwa 1. (Picha na Kassim Mbarouk) 
Ubao wa matokeo, ulivyokuwa ukisomeka hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa ya mchezo kati ya timu hizo leo jioni, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Jean Paulsen, akimpongeza mchezaji Mwinyi Kazi Moto, mara baada ya kumalizaka kwa  mchezo kati ya timu hizo leo jioni, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment