TANGAZO


Saturday, February 11, 2012

Simba yairarua Azam FC Taifa


Emmanuel Okwi wa Simba akitafuta mbinu ya kumtoka Said Morad wa Azam FC, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Simba ilishinda mabao 2 - 0. (Picha na Kassim Mbarouk)


Emmanuel Okwi wa Simba akitafuta mbinu ya kumtoka Agrey Ambross wa Azam FC (kushoto) na Abdi Kassim (katikati), wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo huo. 


 Mashabiki wa Azam FC, wakiishangilia timu yao katika mchezo huo.


 Mashabiki wa Simba, wakishangilia moja ya bao, lililofungwa na Emmanuel Okwi, aliyefunga mabao yote mawili ya timu hiyo katika mchezo huo.


 Felix Sunzu wa Simba, akitafuta mbinu ya kumtoka Said Morad wa Azam FC (15).


 Salum Abubakar wa Azam FC, akimtoka Juma Jabu wa Simba.

Wachezaji wa Simba, wakiongozwa na Nahodha wao, Juma Kaseja, wakishangilia ushindi wa mabao 2 - 0, mara baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo huo.

No comments:

Post a Comment