TANGAZO


Wednesday, February 8, 2012

NECTA yatangaza matokeo Kidato cha Nne na QT


Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako, akitangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne na QT, leo Februari 8,2012. (Picha na Kassim Mbarouk)
Na Kassim Mbarouk
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dk. Joyce Ndalichako, leo, ametangaaza rasmi matokeo ya mitiahani ya Maarifa (QT) na ile ya kidato cha nne (CSEE), iliyofanyika mwezi Oktoba 2011.
Akitangaza matokeo hayo, Dk. Ndalichako, alisema kuwa kwa matokeo ya mtihani ya maarifa (QT), kumekuwepo na ongezeko la ufaulu kwa wastani wa asilimia tano, ikilinganishwa na ule wa mwaka juzi, ambapo walifaulu kwa wastani wa asilimia 35 na sasa asilimia 40.
Alisema kuwa katika mtihani huo wa 2011, watahiniwa waliosajiliwa walikuwa ni 29,447, ambapo wasichana walikuwa ni 18019 na wavulana 11428, ambapo waliofanya mtihani huo, walikuw ni
watahiniwa 22,400, ikiwa ni sawa na asilimia 76.07 ya waliosajiliwa waliofanya mtihani. Kati ya hao
wasichana waliofanya mtihani ni 13,898 na wavulana wakiwa ni 8,502.
Aidha, alisema jumla ya watahiniwa 9,069 sawa na asilimia 40.70 ya waliofanya mtihani wamefaulu,
ikilinganishwa na asilimia 35.17 ya waliofaulu mtihani wa maarifa 2010 na hivyo kiwango cha ufaulu kuongezeka kwa asilimia 5.53.
Ama kwa ule wa kidato cha nne (CSEE) 2011, alisema kuwa jumla ya vituo 4,795 vilitumika katika kufanya mtihani huo, ikilinganishwa na vituo 4,653 vilivyotumika mwaka 2010.
Alisema usajili wa mahudhurio kwa mtihani wa CSEE, jumla ya watahiniwa 450,324, walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne 2011, wakiwemo wasichana 201,799 sawa na asilimia 44.81 na wavulana 248,525 sawa na asilimia 55.19 na kuasema kuwa kiwango cha watahiniwa kwa mwaka 2011, kimeshuka ikilinganishwa na mwaka wa 2010 ambapo watahiniwa waliosajiliwa walikuwa ni 458,114 na hivyo kupungua watahiniwa 7,790 ambapo ni sawa na asilimia 1.70.
"Watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2011 ni 426,314 sawa na asilimia 94.67. Watahiniwa 24,010 hawakufanya mtihani, sawa na asilimia 5.33 ya watahiniwa wote waliosajiliwa," alisema.
Kwa upande wa watahiniwa wanaotoka mashuleni, alisema waliosajilwa walikuwa ni 349,390 kati yao wakiwemo wasichana 150,371 ambao ni sawa na asilimia 43.04 na wavulana 199,019, ikiwa ni sawa na asilimia 56.96. Mwaka 2010 watahiniwa wa shuke walikuwa 363,589 na hivyo kusema kuwa idadi ya watahiniwa wa shule imepungua kwa 14,209, sawa na asilimia 3.91, ikilinganishwa na idadi ya waliosajiliwa 2010.
Alisema kuwa watahiniwa wa shule waliofanya mtihani, walikuwa 339,330, sawa na asilimia 97.12. Watahiniwa 10,060, sawa na asilimia 2.88, hawakufanya mtihani.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea,waliosajiliwa alisema kuwa walikuwa 100,934, wakiwemo wasichana 51,428 sawa na asilimia 50.95 na wavulana 49,506 sawa na asilimia 49.05 mwaka 2010, watahiniwa wa kujitegemea, waliosajiliwa walikuwa 94,525. Hivyo, alisema kuwa idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa 6,409, sawa na asilimia 6.78, ikilinganishwa na idadi ya
waliofanya mtihani huo, mwaka 2010.
Kwa upande wa watahiwa wa kujitegemea, waliosajiliwa walikuwa ni 100,934, wakiwwemo wasichana 51,428, sawa na asilimia 50.95 na wavulana 49,506, sawa na asilimia 49.05. Mwaka 2010,
watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 94,525. Hivyo idadi ya watahiniwa imeongezeka kwa 6,409, sawa na asilimia 6.78, ikilinganishwa idadi ya waliofanya mtihani huo mwaka 2010.Watahiniwa 86,984, wakiwemo wasichana 44,639 na vulana 42,345, wamefanya mtihani.
Watahiniwa wa kujitegemea 13,950, sawa na asilimia 13.82, hawakufanya mthani.
Kwa upande wa matokeo ya kidato cha nne, Dk. Ndalichako, alisema kuwa jumla ya bwatahiniwa 225,126, sawa na asilimia 53.37, wamefaulu mtihani huo, 2011, wakiwemo wasichana 90,885, sawa
na asilimia 48.25 ya wasichana waliofanya mtihani na wavulana 134,241, sawa na asilimia 57.51 ya wavulana waliofanya mtihani. Mwaka 2010, watahiniwa waliofaulu walikuwa 223,085,
sawa na asilimia 50.74. Hivyo, alisema kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.63.
Kwa upandea wa watahiniwa wa shule, Dk. Ndalichako, alisema kuwa jumla ya watahiniwa 180,216, sawa na asilimia 53.59 ya waliofanya mtihani wa kidato nne 2011, wamefaulu. Kati ya hao
wasichana wakiwa ni 69,913, sawa na asilimia 44.36 na wavulana wakiwa ni 110,303, sawa na asilimia 53.53.
"Mwaka 2010 watahiniwa waliofaulu mtihani huo, walikuwa 177,021, sawa na asilimia 50.40 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 2.63," alisema.
Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, alisema idadi ya waliofaulu mtihani huo, ilikuwa ni
44,910, sawa na asilimia 52.52 ya waliofanya mtihani, kati yao, wasichana wakiwa ni 20,972, sawa na asilimia 47.90 na wavulana wakiwa ni 23,938, sawa na asilimia 57.38.
"Mwaka 2010, watahiniwa wa kujitegemea 46,064, sawa na asilimia 52.09, walifaaulu mtihani huo," alisema Dk. Ndalichako.
Kwa upande wa udanganyifu kwenye mitihani hiyo, alisema kiwango cha udanganyifu kimeongezeka na kuzitaja mbinu mbalimbali zinazotumiwa na baadhi ya watahiniwa hao.Dk. Ndalichako, alizitaja baadhi ya mbinu hizo kuwa ni pamoja na kuweka maandishi ya majibu kwenye mapaja kwa upande wa wasichana na vikaratasi kwenye kola za tai kwa wavulana.

No comments:

Post a Comment