Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo asubuhi, Februari 8, 2012, wakati alipokuwa akitangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha Nne na Maarifa (QT), ofisini kwake, Kijitonyama jijini. (Picha na Kassim Mbarouk)
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, akitangaza matokeo hayo. Kushoto ni baadhi ya Maofisa na Wakurugenzi wa Wizara ya Elimu na Baraza hilo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipokuwa akitangaza matokeo hayo. Kulia ni baadhi ya waandishi hao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, akiwaonesha waandishi wa habari, rula ambazo baadhi ya watahiniwa wa kidato cha nne, walikuwa wameandika majibu ikiwa ni moja ya udanganyifu, aliosema kuwa uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watahiniwa hao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, akiwaonesha waandishi wa habari, counterbook, ambalo alisema kuwa alikamatwa nalo mmoja wa watahiniwa, akijisomea wakati akiwa ameaga kwenda kujisaidia kwenye vyoo vya moja ya vituo vya kufanyia mitihani hiyo.
Dk. Ndalichako, akionesha picha za watahiniwa ambazo alisema huzitumia kwa ajili ya kuwatambua watahiniwa waliomaliza miaka ya nyuma, ambao hufanya kazi ya kuwafanyia watahiniwa wapya mitihani yao.
Dk. Ndalichako, akionesha moja ya udanganyifu, aliosema ni wa hali ya juu kwani alisema majibu yao watahiniwa wote yalikuwa yamefafana kwa yale waliyoyapata na yale waliyokosea.
Dk. Ndalichako, akionesha tofauti ya majibu ya watahiniwa hao na wale ambao walikuwa wakifanya bila udanganyifu.
Dk. Ndalichako akielezea zaidi waandishi wa habari, namna udanganyifu wa watahiniwa unavyozidi kuongeza kila mwaka, ambapo amewashukuru baadhi ya wasimamizi wa vituo kwa ujasiri wao kwa watahiniwa wasio waaminifu.
Dk. Ndalichako akionesha tofauti za mwandiko wa mtahiniwa aliyekuwa akisaidiwa kufanya baadhi ya majibu na mtahiniwa mwenzake na jinsi walivyoweza kummbaini aliyekuwa akimsaidia.
Dk. Ndalichako, akionesha moja ya karatasi ya majibu ya mtahiniwa aliyekuwa akifanya vizuri kwenye masomo yake ya kila siku lakini akashindwa kufanya chochote kwenye mitihani yake hiyo.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, waliokuwa wakifuatilia matokeo hayo, yaliyokuwa yakitangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako, leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako, akioneshwa moja ya kielelezo cha mkono wa shati, alichokamatwa nacho mmoja wa watahiniwa, akiwa ameandika majibu ya moja ya mitihani hiyo. Kushoto ni Naibu Katibu Mtendaji wa Baraza, Dk. Charles Msonde na kulia ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala, Daniel Mafie.
No comments:
Post a Comment