Watu wanane wamekamatwa Uingereza katika uchunguzi kuhusu malipo ya rushwa kwa polisi na maafisa wa serikali.


Kati ya waliokamatwa ni wafanyakazi watano wa gazeti linalouza sana nchini Uingereza, The Sun, afisa mmoja wa polisi, mwanajeshi, na mfanyakazi mmoja wa Wizara ya Ulinzi.
Taarifa iliyotolewa na kampuni ya gazeti hilo, News Corporation, ilisema iliipa polisi habari zilizopelekea watu hao kukamatwa.