TANGAZO


Friday, June 8, 2018

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU, ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITA ZA LUKU ZA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akiwa ameshika moja ya mita ya kisasa ya LUKU (Smart Meter), iliyotengenezwa na kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam, wakati alipokitembelea kujionea mita hizo leo Juni 8, 2018.
NA K-VIS BLOG/KhalfanSaid
NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, ametembelea kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam leo Juni 8, 2018 na kuridhishwa na ubora wa mita hizo.
Alisema tatizo la mita lilikuwa ni changamoto kubwa iliyopelekea kasi ya kuwafikishia umeme Watanzania kuwa na kikwazo kwani TANESCO iliagiza mita hizo kutoka nje.
Kampuni ya Baobab Engineering System Tanzania ndiyo watengenezaji wa mita hizo za kisasa za  LUKU (Smart Meters) na uongozi wa kiwanda umeahidi kuzalisha mita za kutosha ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiikabili TANESCO kuhusu upatikanaji wa mita.
“Sisi katika kutaka shirika letu la TANESCO lifanye vizuri tumewapa maelekezo yako ndani ya Sera na mipango yetu lazima waunganishie umeme wateja wengi na moja ya component inayotakiwa ni mita, kumekuwa na changamoto ya mita kama mlivyosema, na hasa inatokana na utaratibu wa uagizaji na hata kufika kwa vifaa hivyo ilichukua muda sana, sasa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mita hapa nyumbani ninaamini tatizo hili sasa halitakuwepo.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu.
Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko Mhandisi Theodory Bayona amesema, tayari Shirika limeanza kutekeleza agizo hilo la serikali na mchakato wa manunuzi umeanza kwa kuhakikisha vifaa vyote vya Shirika vinanunuliwa kutoka ndani na tayari TANESCO imeanza kwa kununua nguzo za umeme hapa hapa nchini, lakini kuhusu mita za umeme TANESCO inampango wa kununua mita 350,000 kutoka kwa wawekezaji wa ndani na mita hizo hasa zitatumika kubadilisha zile mita zile za zamani ambapo zilikuwa haziendi sawasawa lakinin pia kuwaunga na wateja wapya., Alisema Mhandisi Bayona.
Awali Mhe. Naibu Waziri alipatiwa maelezo ya kiuntendaji ya kiwanda hicho kabla ya kupata fursa ya kutembelea eneo la uzalishaji na kujionea jinsi mafundi wazawa wa kiwanda hicho wanavyotengeneza mita hizo la LUKU.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizunguzma jambo baada ya kujionea mita hizo.
Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
Mhe. Naibu Waziri akiangalia utaalamu wa kutengeneza mita hizo.
Mhe. Naibu Waziri akiangalia utaalamu wa kutengeneza mitab hizo.
Moja ya mita hizo ikiwa katika hatua za mwisho za matengenezo.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
Mhe. Subira Mgalu, akizunhuzma. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhhulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania, Bw. Allan Magoma, akizungumza.
Picha ya pamoja. 

No comments:

Post a Comment