Mwanamume mmoja katika jimbo ya Texas, Marekani nusura afe baada ya kuumwa na kichwa cha nyoka ambaye alikuwa amemkata na kumuua.
Jennifer Sutcliffe ameambia kituo cha runinga cha KIII-TV kwamba mumewe alikuwa akifanya kazi shambani pale alipomuona nyoka huyo wa urefu wa futi nne (1.25m) na kumkata kichwa kwa upanga.
Nyoka huyo alikuwa aina ya nyoka atoae sauti ya kuchacharika kwa mkia wake, maarufu kwa Kiingereza kama rattlesnake.
Alipouchukua mzoga wa nyoka huyo akautupe, kichwa cha nyoka huyo kilimuuma.
Ililazimu madaktari kumdunga sindano ya vipimo 26 vya dawa ya kuua sumu kumuokoa.
Nyoka akiguswa anaweza kumuuma mtu saa kadha kabla ya nyoka huyo kufa.
Bi Sutcliffe ameambia KIII-TV kwamba mumewe alianza kupapatika ghafla.
- Nyoka 'watoroka' katika shamba China
- Nyoka atafuta 'joto' kwenye kiatu
- Nyoka apatikana kwenye ndege Marekani
Alisafirishwa kwa ndege hadi kwenye hospitali iliyo karibu na Corpus Christi ambapo alitibiwa kwa dawa ya kuua sumu aina ya CroFab.
Wiki moja baada ya kisa hicho, mwanamume huyo anadaiwa kuwa katika hali nzuri hospitalini, ingawa figo zake bado ni dhaifu.
Leslie Boyer, ambaye ni daktari wa kukabiliana na sumu ya nyoka katika taasisi ya VIPER ya chuo kikuu cha Arizona amewatahadharisha watu dhidi ya kujaribu kuwaua nyoka, hasa kwa kuwakata kata.
"Ni ukatili dhidi ya wanyama hao na hukuacha na vipande vingi vyenye sumu ambavyo unahitaji kuviokota," aliambia tovuti ya Gizmodo.
No comments:
Post a Comment