TANGAZO


Sunday, June 10, 2018

Mtaalamu bingwa wa afya ya akili kutoka Tanzania kutuzwa Marekani

Sylvia Kaaya


Haki miliki ya pichaSYLVIA KAAYA
Image captionSylvia Kaaya

Mtaalam bingwa wa kukabiliana na matatizo ya kiakili na mtafiti kutoka Tanzania Profesa Sylvia Kaaya ni miongoni mwa watu sita ambao watatuzwa shahada ya heshima na chuo cha Marekani cha Dartmouth.
Profesa Kaaya kutoka chuo cha Afya na Sayansi cha Muhimbili (Muhas), ni miongoni mwa wataalam 60 wa kukabiliana na matatizo ya kiakili nchini Tanzania anayeangazia kuendeleza vitendo vinavyoweza kufaidi mataifa yalio na raslimali chache, kulingana na duru za gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Ripoti iliotolewa na chuo hicho cha zamani, nchini Marekani,The Darmouth kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Profesa Kaaya alihusishwa na taasisi ya Dartmouth kupitia ushirikiano wa DarDar ambao ulianzishwa 2001 ili kuunganisha Geisel na chuo kikuu cha Muhimbili kukabiliana na maswala ya Afya duniani.

Image captionChuo kikuu cha Muhimbili nchini Tanzania

Chuo kikuu cha Muhimbili nchini Tanzania Dartmouth inatarajiwa kuwatuza shahada hizo watu sita katika sherehe itakayofanyika Juni 10 .
Kila anayetuzwa atapewa shahada ya heshima ya Udaktari.
Taaluma za wataalam hao zinaangazia maswala tofauti kutoka burudani, huduma kwa jamii hadi matibabu.
Miongoni mwa wale watakaotuzwa ni pamoja na wadhamini wa taasisi hiyo pamoja na mshirika wa Goldman Sachs aliyestaafu Peter fahey, mbunge wa zamani na mwakilishi katika Umoja wa mataifa Frank Guarini ambaye ni afisa wa matibabu pamoja na daktari wa upasuaji Williams Holmes, Muigizaji , mtayarishaji na mwandishi Mindy Kaling na Mwanzilishi pamoja na mwenyekiti wa kampuni ya Carlyle David Rubenstein.

No comments:

Post a Comment