Baadhi washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya wasindikaji wadogo wa vyakula mkoani Tabora wakifuatilia mafunzo jana ya kuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha bidhaa zitakazokuwa na ubora na usalama utawawezesha kupata soko ndani na nje ya nchi.(Picha zote na Tiganya Vincent.)
Katibu wa washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya wasindikaji wadogo wa vyakula mkoani Tabora Raphael Francis akisoma risala jana ya Wasindikaji wakati wa kufunga yao ambayo yamewajengea uwezo ili waweze kuzalisha bidhaa zitakazokuwa na ubora na usalama utawawezesha kupata soko ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya wasindikaji wadogo wa vyakula mkoani Tabora Amina Madeleka akitoa neno la shukurani jana kwa TFDA kwa kuwapa mafunzo Wasindikaji ambayo yamewajengea uwezo ili waweze kuzalisha bidhaa zitakazokuwa na ubora na usalama utawawezesha kupata soko ndani na nje ya nchi.
Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Dkt. Edger Mahundi akitoa ufafanuzi wa maeneo ambayo wamewafundisha wasindikaji wadogo wa chakula ambayo yalilenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa ambazo ni bora na salama kwa ajili ya kupata soko ndani na nje ya nchi wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika mkoani Tabora.
Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Justin Makisi akitoa maneno ya utangulizi jana wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya siku mbili ya wasindikaji wadogo wa chakula mkoani Tabora yalikuwa yakiwajengea uwezo wa kuweza kusindika chakula kilicho katika ubora na usalama kwa lengo kupanua masoko yao.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya siku mbili ya wasindikaji wadogo wa vyakula mkoani Tabora Amina Madeleka akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo yaliyokuwa yakiwajengea uwezo wa kuweza kusindika chakula kilicho katika ubora na usalama kwa lengo kupanua masoko yao.
Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu ) Hajjat Rukia Manduta akifunga mafunzo ya siku mbili jana ya wasindikaji wadogo wa chakula mkoani Tabora yalikuwa yakiwajengea uwezo wa kuweza kusindika chakula kilicho katika ubora na usalama kwa lengo kupanua masoko yao.
Na Tiganya Vincent, RS Tabora
7 June 2018
UONGOZI wa Halmashauri za Wilaya zote Mkoani Tabora zimataka kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya Wasindikaji wadogo wa vyakula kuwa na mazingira mazuri ambayo yatawafanya wazingatie taratibu bora za usindakaji na usafi wa mazingira ya uzalishaji ili bidhaa zao wanazozalisha ziweze kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Hajjat Rukia Manduta wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa ambazo zitawawesha kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi.
Alisema eneo hilo litawawezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa na mamlaka nyingine kuweza kuwatembelea kwa urahisi na kuwapa ushauri ambao utawasaidia kupanua uzalishaji wao.
Aidha Hajjat Rukia aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia elimu waliyopata katika uzalishaji bidhaa bora na salama zenye ushindani kwenye la ndani na nje ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya ujenzi wa viwanda.
Aliongeza kuwa ni vema wakatumia mafunzo hayo kuwa mabalozi wa utoaji wa elimu kwa wasindikaji wengine ambao hawakuhudhuria ili nao wanasindika chakula wazingatie usalama, usafi na usindikaji wa kisasa kwa kuongezea thamani bidhaa zao.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Justin Makisi alisema baada ya mafunzo waliyopatawashiriki hao hatarajii kuona tena bidhaa hafifu kutoka Tabora zikiwa sokoni.
Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo kutoka Wilayani Sikonge Raphael Francis aliiomba Serikali kupunguza tozo ya vifungashio ili wasindikaji wengi watumie vifungashi vilivyo safi na salama.
No comments:
Post a Comment