TANGAZO


Tuesday, June 5, 2018

BUNGE LAIDHINISHA BAJETI YA TRILIONI 12.058 KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA 2018/19

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakifuatilia kwa makini michango ya Wabunge wakati wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo kabla haijaidhinishwa Bungeni Jijini Dodoma. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, wakifurahia jambo wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango, iliyopitishwa na Bunge, Jijini Dodoma.  
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akitoa majumuisho ya hoja za Waheshimiwa wabunge kuhusu Wizara hiyo  kabla ya kuidhinisha Bajeti yake ya shilingi trilioni 12.058, ambapo shilingi trilioni 10.763 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.295 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2018/19.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akionesha kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa wa Taifa wa Miaka Mitano, wakati wa kuhitimisha hoja za Wabunge kuhusu bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango Bungeni, Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu hoja za Wabunge kuhusu Uhimilivu wa Deni la Taifa ambapo alieleza kuwa bado Deni hilo ni himilivu kwa vigezo vya kimataifa.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za Wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara yake Bungeni Dodoma.  
Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya Bajeti ya Wizara hiyo, ya shilingi trilioni 12.058, kuidhinishwa na  Bunge, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (tai ya rangi ya Bendera ya Taifa), viongozi wengine wa Wizara hiyo na Maafisa Waandamizi wa wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Bunge kuridhia na kuidhinisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19.  
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), viongozi wengine wa Wizara hiyo na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakishangilia baada ya Bajeti ya Wizara hiyo kuidhinishwa na Bunge. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Dodoma)

No comments:

Post a Comment