TANGAZO


Friday, April 27, 2018

TAARIFA YA CUF KWA UMMA KUHUSU MASHAURI YA CHAMA YANAYOENDELEA MAHAKAMANI MWEZI APRIL/MAY, 2018


THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

THE DIRECTORATE OF INFORMATION,
PUBLICITY AND PUBLIC RELATION

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU MASHAURI YA CHAMA YANAYOENDELEA MAHAKAMANI MWEZI APRIL/MAY, 2018

LEO MBELE ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Dyansobera, Mahakama Kuu imetupilia mbali Pingamizi lililowekwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata na Jopo lake kutoka Ofisi ya AG katika Shauri Namba 80/2017 lililofunguliwa na THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) dhidi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini (Jaji Franscis Mutungi), na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Mheshimiwa Joran Lwehabura Bashange ndiye aliyeiwakilisha THE REGISTERED TRUSTEES..( Bodi ya Wadhamini ya CUF) kwa maana ya Kusaini nyaraka zote za Mahakama (Drawer) na kuwa Muwakilishi katika shauri hili ambalo hakuweka Wakili.

Mhe. Bashange kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya CUF anaiomba Mahakama Kuu kutoa amri ya Kumzuia Msajili Jaji Mutungi kutotoa fedha za Ruzuku ya CUF kwa Lipumba na Genge lake mpaka hapo shauri la msingi Namba 68/2017 litakaposikilizwa na kutolewa Maamuzi.
Shauri hili linakuja kwa kutajwa Tarehe 3 May, 2018.

Wakili wa Serikali aliweka mapingamizi mawili moja amedai kuwa;
Maombi hayapo sahihi kuwasilishwa mahakamani kwa kuwa hayana maamuzi ya bodi (Body Resolution) na Pili,

Muwasilisha maombi (Bashange) hana Mamlaka kisheria (Locus Stand) kufungua shauri hilo Mahakamani.

Katika ufafanuzi wake amedai kuwa Mhe Bashange sio muombaji (Applicant), wala sio Wakili (Advocate) na Wala hajapewa nguvu ya kisheria kufungua shauri hili na mamlaka husika (Recognized persons who have Power of Attorney) hivyo haruhusiwi kuandaa nyaraka (Draw), kuwakilisha mahakamani (Appear to the Court) na kuwasilisha (To present any Claims), na kwamba Hakuna Maamuzi yeyote ya vikao iliyomuidhinisha (Body Resolution).    

Mhe.Bashange alijibu hoja zote hizo kwa ufasaha mkubwa kama [Learned Advocate] na kueleza kuwa Bodi ya Wadhamini ni “Corporate entity” yenye “Legal Personality” kwa mujibu wa sheria ya Udhamini kifungu cha 21 na Sheria ya Vyama vya siasa 318 (2002). Bashange aliiambia Mahakama kuwa sheria haielezi nani anayepaswa kuleta shauri Mahakamani. Na kutoa vielezo vya kutosha vya rejea ya maamuzi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaani kukazia hoja zake.

MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU:

Mhe. Jaji alieleza kuwa Mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili. Rejea za ushahidi zilizonukuliwa na kuzingatia Msimamo wa Maamuzi ya Mahakama ya Rufaani kuhusu tafsiri na maana ya Locus Stand and Body Resolution. Pia, Mhe. Jaji alieleza nini maana ya Pingamizi la Awali (Preliminary Objections). Locus Stand and Body Resolution.

Ameeleza kuwa Msimamo wa Mahakama ya Rufaani ni kwamba HAKUNA/HAIRUHUSIKI KUWEKWA PINGAMIZI JUU YA ‘LOCUS STAND’. Ameeleza kuwa mtu hawezi kukurupuka kuja mahakamani kuleta shtaka (Case) hivi hivi tu. Lazima kuna sababu. Mahakama inatakiwa kusikiliza ni kwa vipi na kwa nini (How and Why?) Shauri limeletwa.

Kuhusu “Body Resolution” ameeleza kuwa; Mahakama imeweka misingi ya kuangalia juu ya kwanza, uwepo wa kampuni husika (existence of Company), Pili, yawepo maamuzi yaliyofikiwa kwa mujibu wa Katiba/ Articles za kampuni, Tatu, kuzingatia kulinda haki za mlalamikiwa, na Nne, kuzingatia kuepuka madhara ya msingi yanayoweza kujitokeza. Wakati ikitafakari kusikiliza au kutosikiliza shauri lililowasilishwa mbele yake na linapojitokeza suala la kuhoji juu ya uwepo wa [Body Resolution].

Mhe Jaji ameeleza kuwa Mahakama imezingatia mambo mawili kufikia maamuzi yake;

Moja, Haki haipaswi kufungwa kutokana na sababu za kiufundi (Justice should not Tied by Technical Reasons) na Pili,

kwamba kila kesi ina upekee wake na mazingira yake (every case is unique and it can only provide the Guidance to decision).

Mahakama imeeleza kuwa suala la kisheria kuhusu mamlaka Halali ya kutoa idhini ya kufunguliwa kwa shauri na bodi ya wadhamini (Dully Authorized) suala hilo linazaa suala la pili Je kama (ndani ya CUF) kuna Bodi Halali ya Wadhamini? Suala hilo ili kulibaini pia inahitajika kufanyika kwa uchunguzi. Kuhitajika uchunguzi kunaondoa sifa ya kuwa Pingamizi. Kwa sababu Pingamizi lazima iwe na hoja halisi za kisheria bila kuhitajika uchunguzi na au ushahidi. (Legal Objections, Pure based on Point of Laws)

Mahakama imeeleza kuwa;  Linaloonekana hapa ni kwamba Bodi ya Wadhamini ya Chama Kimoja imegawanyika. Ipi Bodi halali inahitaji ufanyike uchunguzi (Inquiry), wapi uchunguzi utafanyika? ni hapa Mahakamani. Suala la Bodi ipi halali ya Wadhamini ya CUF linaendelea kushindaniwa Mahakamani. Mpaka sasa Hakuna Bodi Halali ya Wadhamini ya CUF.

HIVYO BASI; kwa msingi wa Hoja zilizoelezwa hapo juu suala hili haliwezi kuwa Pingamizi la kisheria kwa Maelekezo ya Mahakama ya Rufaani. (If there is an Issue Disputed to the Court, That matter cannot be objected as Preliminary Objection).

MAHAKAMA KUU IMETUPILIA MBALI MAPINGAMIZI HAYO NA KUPANGA RATIBA YA KUSIKILIZA SHAURI HILO KWA NJIA YA MAJIBIZANO YA MAANDISHI MPAKA TAREHE 24 MAY, 2018 NA BAADAE KUTOLEWA MAAAMUZI.

Baada ya Maamuzi hayo na kuanza kupangwa kwa Ratiba ya usikilizwaji wa shauri hilo kwa njia ya maandishi ili kuokoa muda kama yalivyowasilishwa na Mhe Bashange.

Wakili Gabriel Malata alipinga wazo la kusikilizwa kwa maandishi akidai kuwa wapo tayari kusikiliza hata leo. Na kwamba kwa msingi wa maamuzi hayo juu ya Pingamizi lao akaiomba Mahakama iliweke pembeni shauri hili mpaka SHAURI LA MSINGI NAMBA 13/2017 la kuhoji uhalali wa Bodi ya Wadhamini litakapotolewa uamuzi.

Mhe Bashange alipinga hoja hizo kwa madai kuwa shauri hili linajitegemea na kwamba Wakili wa Serikali kama Afisa wa Mahakama anapaswa kuisaidia Mahakama kuzuia uharibifu wa mali za umma (Fedha za Ruzuku za CUF) kufunjwa na Msajili Jaji Mutungi na Lipumba.

Awali, Lipumba na Mawakili wake walijaribu kutaka kuingia katika Shauri hili kwa kuiomba Mahakama imsikilize Wakili wake Mashaka Ngole badala ya Mhe Bashange kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini, Mahakama ikakataa kwa hoja. Baadae kwa mara ya Pili wakafanya jaribio la kutaka kuliondoa shauri hili Mahakamani wakagonga mwamba. Mara ya Tatu, wakaja na suala la kumkataa Jaji na kumuomba ajitoe, nalo wakagonga mwamba, na hii ni mara ya NNE kufanya Jaribio la kuweka Pingamizi ili shauri lisisikilizwe.

PONGEZI NA SHUKRANI ZA DHATI kwa Mawakili Wasomi Hashimu Mziray, Daimu Halfani na Juma Nassoro kwa kazi kubwa ya kumuandaa vyema The Programmed Learned Advocate Honourable Joran Lwehabura Bashange na kuweza kuligalagaza Jopo la Mawakili saba wa Serikali.  

TUKUTANE MAHAKAMA KUU TAREHE 3 MAY, 2018 SAA 3 ASUBUHI

THE NEW, STRONG, AND VIBRANT CUF IS COMING BACK SOON

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa Leo Tarehe 27/4//2018 na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa

SALIM BIMANI
MKURUGENZI -MHUMU
Zantel- 0777414112, Voda- 0752325227

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI-NMHUMU
Tigo-0715 062 577, Voda -0767 062 577

No comments:

Post a Comment