TANGAZO


Tuesday, March 6, 2018

MAMA KIKWETE MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI TABORA

Mama Salma Kikwete

Na Vincent-RS Tabora 
6 March 2018
MKE wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa  Mkoa wa Tabora.

Maadhimisho hayo mwaka huu kimkoa yanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Chipukizi katika Manispaa ya Tabora na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi alisema katika maadhimisho hayo wakinamama wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbalimbali mkoani humo watapata fursa ya kuonyesha kazi mbalimbali wanazoshughulika nazo katika kujiletea maendeleo.

Aliongeza kuwa jioni kutakuwepo na Chakula (dinner) ambapo kila mshiriki anatakiwa kuchangia fedha na kuongeza kuwa kutakuwepo na  burudani kutoka kwa wasanii wakubwa akiwemo Hadija Kopa.

No comments:

Post a Comment