Maafisa katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul, wanasema wamemaliza mkwamo wa saa 12 kufuatia shambulio la wanamgambo dhidi ya hoteli kubwa ya Intercontinental.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema raia wasita wameuawa, pamoja na washambuliaji wote watatu.
Ni ishara ya hivi karibuni ya ghasia zinazoendelea kushudiwa nchini Afghanistan.
Usiku kucha, vikosi maalum vilipambana kuidhibiti hoteli hiyo.
- Marekani kuongeza askari Afghanistan
- 30 wafariki katika mlipuko Afghanistan
- Taliban wawaua wanajeshi 26 wa Afghanistan
Zaidi ya watu 150, wakiwemo wageni, walikuwemo ndani ya hoteli hiyo Jumamosi jioni wakati washambuliaji waliojihami kwa bunduki walipoivamia hoteli hiyo na kuanza kufyetuwa risasi.
Televisheni nchini humo zimewaonyesha wageni wakishuka kutoka orofani kwa kutumia matandiko, waliyoyafunga kwenye roshani na kukwepa.
Moshi mkubwa ulitanda usiku angani, ikiwa ni baada ya sehemu ya jengo hilo kuteketezwa moto.
Hoteli hiyo ya Intercontinental ni mojawapo ya majengo makuu ya mji wa Kabul.
Hutumika sana na wageni wa nchi za nje, wanasiasa nchini, hutumika pia kuandaa shrehe za harusi na mikutano.
Ni eneo la wazi linaloweza kulengwa na wanamgambo na lilishambuliwana wapiganaji wa Taliban miaka 7 iliyopita.
Lakini shambulio hili la sasa lililodumu kwa muda mrefu na linaloonekana kuwa gumu, linajiri katika wakati ambapo kuna ongezeko la wasiwasi kuhusu kudorora kwa usalama katika mji mkuu huo, na litazusha maswali kuhusu vipi usalama wa kivitengo katika hoteli hiyo ulivyoweza kuvukwa.
No comments:
Post a Comment