TANGAZO


Sunday, January 21, 2018

Ghasia zazuka kuhusu kura ya Honduras inayokumbwa na mzozo

Maandamano yalipangwa na wafuasi wa mgombea wa upinzani aliyeshindwa

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaandamano yalipangwa na wafuasi wa mgombea wa upinzani aliyeshindwa
Muandamanaji mmoja ameuawa katika mapigano Honduras kati ya polisi ya kupambana na fujo na waandamanaji waliokuwa wanapinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.
Polisi wamefyetua gesi ya kutoa machozi na kuondosha vizuizi barabarani vya matairi yalioteketezwa moto kote nchini. kifo hicho kimetokea katika mji wa kaskazini wa Saba.
Maandamano hayo yalipangwa na wafuasi wa mgombea wa upinzani aliyeshindwa.
Mwezi uliopita, rais aliyepo Juan Orlando Hernandez alitangazwa mshindi licha ya maandamano ya siku kadhaa.
Siku ya Jumamosi shirika lisilo la serikali mjini Saba, limesema mwanamume mwenye umri wa miaka 60 aliuawa na mwingine kujeruhiwa wakati polisi ilipofyetuwa risasi katika kituo cha ukaguzi, shirika la habari la Reuters, limeripoti.
Uchaguzi huo wa November 25 umeshutumiwa pakubwa. Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Salvador Nasralla wana shaka kubwa na tume ya uchaguzi iliyohesabu kura.
Hii ni kwa sababu ilichaguliwa na bunge linalodhibitiwa na chama cha National Party cha Hernández.
Maelfu wamemiminika mjini kuandamana kupinga matokeo ya uchaguziHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaelfu wamemiminika mjini kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi
Awali Nasralla aliongoza katika kura hizo zilipokuwa zinahesabiwa, lakini hilo likabadilika haraka na akaushutumu utawala kwa kubadili matokeo.
Maelfu ya watu waliandamana barabarani katika maandamano ya upinzani kufuatia uchaguzi huo.
Shirika la Amnesty International linasema watu 14 wamefariki katika mapigano, lakini polisi wanasema ni watatu pekee waliouawa.
Rais Hernández, mwenye umri wa miaka 49, amekuwa madarakani tangu 2013, na ni rais wa kwanza kuwania muhula wa pili baada ya mahakama ya juu zaidi ya nchi hiyo kuondosha marufuku ya kuwania muhula wa pili.

No comments:

Post a Comment