TANGAZO


Thursday, January 18, 2018

Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 18.01.2018

Sanchez

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSanchez
Mkataba wa Manchester United kumsaini mshambualiaji wa Arsenal raia wa Chile utagharimu pauni milioni 180 baada ya Sanchez kukubali mkataba wa miaka minne unusu. (Telegraph)
Mkataba wa Sanchez na Manchester United utamlipa mchezaji huyo wa umri wa miaka 29, paunia 400,000 kwa wiki. (Independent)
Liverpool wamewaambia Sevilla kuwa hawako tayari kumnunua mshambuliaji raia wa England Daniel Sturridge, 28 kwa mkopo. (Mail)
Andy CarrollHaki miliki ya pichaPA
Image captionAndy Carroll
Mchezaji anayemezewa mate na Chelsea Andy Carroll aliiambia West Ham kuwa hawezi kufanya mazoezi - lakini klabu hiyo inauliza ni kwa nini licha ya mchezaji huyo kufanyiwa uchunguzi kwenye goti lake. (Mirror)
Manchester United wameanza mazungumzo kuongeza mkataba wa kipa David de Gea, 27. (Telegraph)
Meneja wa West Ham David Moyes alikuwa Stamford Bridge siku ya Jumatano kumtazama mshambuliaji raia wa Ubelgi Michy Batshuayi, ambaye anataka kumsaini. (Mail)
Real Madrid wanaamini kuwa wakati umewadia kuwasaini washambuliaji watatu wakiwemo mshambuliji wa PSG raia wa Brazil Neymar, Eden Hazard wa Chelsea na Robert Lewandowski wa Bayern Munich.(Marca)
Robert LewandowskiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRobert Lewandowski
Bayern pia huenda wakazungumziwa na Everton kuhusu beki raia wa Uhispania Juan Bernat. (Liverpool Echo)
Mwekezaji mkuu raia wa Uingereza ambye alikuwa na mpango wa kumsaidia Amanda Staveley kuinunua Newcastle sasa ameamua kuunga mkono ununuzi huo. (Guardian)
Meneja wa Newscastle Rafael Benitez atafanya hatua mpya ya kumshawishi mmliki Mike Ashley kufadhili ununuzi wa wachezaji wapya mwezi Januari.(Northern Echo)
Rafael BenitezHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionRafael Benitez
Liverpool wana hofu kupoteza kwa Bayern Munich mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka, 22. (Liverpool Echo)
Mlinzi wa Arsenal Hector Bellerin huenda akawa lengo la Juventus msimu huu. Juventus wamekuwa wakimtazama mchezaji huyo wa miaka 24 raia wa Uhispania tangu mwaka 2014. (Tuttosport - in Italian)
Juventus pia wanamtafuta mchezaji wa Tottenham raia wa Denmark Christian Eriksen, 25, au kiungo wa kati mjerumani Mesut Ozil kuwa nambari 10 wao mpya. (Corriere dello Sport - in Italian)
Chelsea wamejiunga na Manchester City na Paris St-Germain katia mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Nice raia wa Ivory Coast Jean-Michael Seri, 26.

No comments:

Post a Comment