Polisi nchini Guinea wanasema kuwa wamemkamata daktari mmoja wa kienyeji kwa kuwalaghai mamia ya wanawake na kuwafanya kuamini kuwa wao ni wajawazito.
N'na Fanta Camara aliwapa wanawake ambao hawakuwa na uwezo wa kuwa wajawazito, dawa ya kienyeji ambayo ilisababisha tumbo zao kufura na kuonekana kuwa wao ni wajawazito.
Kutokana na huduma hizo wagonjwa walilipa dola 33 kwenye nchi ambayo kipato cha kila mwezi kinakadiriwa kuwa dola 48.
Polisi wanaamini kuwa Bi Camara alipata maelfu ya dola kila mwezi licha ya yeye kusema kuwa alijaribu tu kusaidia.
- Utafiti: Uvimbe wa saratani ya matiti huwa ''mkubwa'' kwa wanawake wanene
- Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyetorokea K Kusini apatikana na minyoo
Siku ya Jumanne zaidi ya wanawake 200 waliandamana nje ya kituo cha polisi kwenye mji mkuu wa Guinea Conakry ambapo Bi Camara alikuwa akizuiliwa.
Zaidi ya wanawake 700 walio na kati ya umri wa miaka 17 na 45 wanaamiwa kuathiriwa na matibabu ya Bi Camara.
Idadi hiyo kubwa inaashiria jinsi Guinea na nchi zingine za Afrika zinawategemea madaktari wa kienyeji
Mwaka 2006 shirika la afya duniani lilisema kuwa asilimia 80 ya waafrika walitumia matibabu ya kienyeji
Wanawake hao walisema kuwa Bi Camara aliwashauri wasimuone daktari, na mara alipothibitisha kuwa wamekuwa wajawazito walistahili kumpa kuku na vitambaa kama njia ya kumshukuru.
Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.
Daktari aliyewachunguza 47 kati ya wanawake walioathiriwa alisema wako kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo ya kiafya ya muda mrefu kutokana na matibabu hayo.
Bi Camara hata hivyo anasema kuwa hajafanya lolote baya.
"Ninafanya kazi ngumu sana kuwasaidia wanawake kuweza kutimiza ndoto zao lakini mengine yako mikononi mwa Mungu, aliwambia waandishi wa habari mjini Conakry.
No comments:
Post a Comment