TANGAZO


Monday, January 22, 2018

George Weah aapishwa kuwa rais Liberia, aahidi kutimiza matarajio

George Weah

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Nyota wa zamani wa kandanda duniani George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.
Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.
Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.
Rais Weah alipokuwa anakula kiapo mjini MonroviaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Weah alipokuwa anakula kiapo mjini Monrovia
Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."
Ameahidi kujitolea kuwatumikia raia wa nchi hiyo.
"Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."
Kiongozi huyo ametumia hotuba yake kusifu uhusiano wa karibu kati ya taifa hilo na Marekani na China.
Kadhalika, amezungumza kuhusu Umoja wa Ulaya.
Amesema: „Bila bara Ulaya, Weah hangekuwa amesimama hapa leo."
Weah akinong'onezana na Bi Ellen Johnson Sirleaf Jumapili wakiwa kwenye ibada kanisani MonroviaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionWeah akinong'onezana na Bi Ellen Johnson Sirleaf Jumapili wakiwa kwenye ibada kanisani Monrovia
Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.
Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo katika uwanja wa Samuel Doe viungani mwa mji wa Monrovia.
Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneta katika bunge la Liberia.
Aligombea urais mwaka 2005, na alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.

No comments:

Post a Comment