TANGAZO


Saturday, November 25, 2017

SERIKALI YATARAJIA KUTOA LESENI KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA VYA UMMA VITAKAVYOKIDHI VIGEZO VYA UBORA

Naibu Waziri, Dkt. Ndugulile akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dkt. Furaha Mwakafyila Ngao baada ya kuibuka mshindi wa Huduma za afya katika vituo vya afya.
Afisa Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Salumu Palango akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wake baada ya kupokea ngao.
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt. Mohamed Mohamed akielezea tathimini ilivyofanyika katika Mkoa huo mwaka 2016 na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Kuibuka mshindi kwa kupata ngao na cheti.
Mkuu wa Wilaya,Evod Mmanda akiongea wakati wa mkutano huo.
Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati)akiongea na Viongozi na Watendaji wa Afya Afya Mkoa na Wilaya ya Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao na vyeti kwa  vituo vya afya vilivyo na ubora wa huduma za afya.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Evod Mmanda na kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Wedson Sichalwe.
Naibu Waziri, akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuibuka mshindi. Dkt. Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara.
Naibu Waziri, Dkt. Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo Manispaa ya Mtwara, ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa. 

No comments:

Post a Comment