TANGAZO


Thursday, November 23, 2017

Man United yalazwa na Fc Basel vilabu bingwa

Lang akifunga krosi iliopigwa na Raoul Petretta.

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionLang akifunga krosi iliopigwa na Raoul Petretta.
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa kikosi chake kilifaa kufunga mabao matano ama sita kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza cha mechi yao ya klabu bingwa waliopoteza kwa Basel.
United ilitawala kipindi cha kwanza cha mechi hiyo huku Marouane Fellaini na Marcos Rojo wakipiga mwamba wa goli.
Lakini licha ya kupata pointi moja walihitaji kufuzu katika raundi ya muondoano na kufikia dakika ya 89 Manchester United walishangazwa na bao la Michael Lang.
"Kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri zaidi, bila mabao siwezi kueleza. Siwezi kuwalaumu wachezaji , alisema Mourinho. Nadhani tunacheza mechi kama hii mara kumi, mara tisa tunashinda bila wasiwasi.Tunapoteza moja na hiyo ndio hii''.
Renato Steffen na Dimitri Oberlin alikuwa amekaribia kuwaweka Basel kifua mbele katika kipindi cha pili kabla ya Lang akifunga krosi iliopigwa na Raoul Petretta.
Sasa itawalazimu klabu ya SCKA Moscow kufunga zaidi ya mabao sita ili kuwafungia Manchester United mnamo tarehe tano mwezi Disemba.

No comments:

Post a Comment