TANGAZO


Tuesday, November 21, 2017

Madereva walevi kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti Kenya?

Chumba cha kuhifadhia maiti
Image captionChumba cha kuhifadhia maiti
Mamlaka ya usalama wa uchukuzi nchini Kenya NTSA imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.
Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za barabarani.
''Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria'', alisema mkurugenzi wa mamlaka hiyo Francis Meja.
Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini.
Image captionHivi ndivyo raia walivyotoa maoni yao baada ya pendekezo hilo la NTSA

No comments:

Post a Comment